NYOSSO KAZOEA HAKA KAMCHEZO, TAZAMA JINSI ALIVYOSHUKIWA NA WADAU WA SOKA AKIWEMO RAIS WA TFF

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Mchezaji na nahodha wa timu ya Mbeya City Juma Nyoso ameendelea kufanya vitendo ambavyo si vya kiungwana na vinavyohitaji kupingwa kwa nguvu zote kwenye soka si la Tanzania pekee bali duniani kote ambako mchezo huu unachezwa.
Nyoso amemfanyia kitendo cha udhalilishaji mchezaji na nahodha wa Azam FC John Bocco ‘Adebayo’ wakati wa mchezo wa timu ya Azam FC dhidi ya Mbeya City uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi ambapo Azam FC waliiibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kitendo kilichofanywa na Juma Nyoso ni cha kulaaniwa na kupigwa vita kwasababu kinaharibu maana halisi ya mchezo wa soka ambao ni wa kistaarabu unaochezwa na waungwana wapenda amani lakini kwa beki huyu wa Mbeya City haiko hivyo.
Msimu uliopita Nyoso alimfanyia kitendo kama alichokifanya leo kwa John Bocco aliyekuwa mshambuliaji wa Simba kwa wakati huo Elius Maguri ambaye kwa sasa anakipiga Stand United ya Shinyanga. Mazingira ya matukio hayo mawili yanafanana kwa asilimia nyingi.
Beki huyo wa zamani wa Simba SC alifanya tukio hilo wakati mpira ukiwa umesimama kama ilivyokuwa kwa Maguri msimu uliopita. Tukio la kumdhalilisha Maguri lilipelekea Nyoso afungiwe kucheza mechi nane za ligi kuu Tanzania bara.
Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya Elius Maguri msimu uliopita wakati Maguri akicheza kwenye klabu ya Simba SC
Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya Elius Maguri msimu uliopita wakati Maguri akicheza kwenye klabu ya Simba SC
Nyoso aliomba radhi kwa kamati ya maadili ya TFF na kwa Maguri pia lakini aliahidi kuorudi kitendo kama hicho kwa siku zijazo.
Lakini ukiwa ni msimu mmoja tu umepita tangu Nyoso apewe adhabu kwa kosa la kumdhalilisha Maguri, leo amerudia kosa lilelile kwa mazingira yaleyale akiwa amevaa kitambaa cha unahodha wa timu ileile.
Hapa napata mashaka na tabia za Nyoso na kujiuliza maswali mengi kichwani moja ya maswali hayo ni kama Juma Nyoso yuko timamu kichwani au la! Nadhani pia anahisi ufahari au ushujaa kufanya vitendo visivyokubalika kwenye soka.
Napata mashaka pia na malezi pamoja na mazingira aliyolelewa Nyoso kutokana na vitendo vyake ambavyo naweza nikaviita ni vya ajabu. Haiwezekani mchezaji yuleyule akafanya vitu vilevile ndani ya muda mfupi huku akiwa ametoka kwenye adhabu ya kosa kama hilo ndani ya miezi michache iliyopita.
Si dhani kama mtu huyu anastahili hata kuvaa kitambaa cha unahodha wa timu kwasababu nahodha ni kiongozi wa wachezaji ndani na nje ya uwanja. Sijui anawaonesha wachezaji wa Mbeya City na watanzania kuwa yeye ni kiongozi wa aina gani.
Awali alifungiwa mechi nane na kusababisha kuyumba kwa timu yake kwasababu inamtegemea kwa kiasi kikubwa uwanjani. Timu hii ndiyo inatoa mshahara kumlipa mchezaji huyu ambaye kukosekana kwake uwanjani kwasababu za kijinga kunapelekea timu kufanya vibaya.
Nyoso ni mchezaji mwenye mzoefu na amecheza timu kubwa pamoja na timu ya taifa, amecheza mechi nyingi za kimataifa na anajua maana ya kuwa mzoefu kwenye timu. Hatukutegemea vitendo kama hivi vifanywe na mtu kama yeye tena mara mbili kwa watu tofauti.
Ili kulinda nidhamu ya soka na wachezaji, TFF inabidi ichukue hatua kali na za haraka kwa Nyoso kwasababu si kitendo cha kwanza kufanywa kwa mchezaji huyo. Safari hii adhabu iwe kali zaidi ili kuzuia tabia chafu kama hizi zinazolishusha soka letu ambalo watu wanapambana kusogea mbele lakini wengine wanatuvuta nyuma.
Tweet y6 Rais wa TFF Jamal Malinzi juu ya tukio lililofanywa na Nyoso dhidi ya John Bocco
Tweet ya Rais wa TFF Jamal Malinzi juu ya tukio lililofanywa na Nyoso dhidi ya John Bocco
Nampongeza Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi kwa kuwa mtu wa mwanzo kabisa kulikemea jambo hili kupitia account yake ya twitter mara baada ya kuona kitendo kilichofanywa na Nyoso na kuahidi kuchukua hatua kali kwa mhusika wa tukio hilo.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top