Manchester United wamekuwa wakikosolewa sana juu ya sera yao ya usajili katika kipindi miaka kadhaa sasa, hasa chini ya utawala wa Louis van Gaal na Ed Woodward. Man United imetumia zaidi ya robo billioni ya paundi za kiingereza tangu LVG alipoanza kazi June 2014. Inaonekana wazi linapokuja suala la usajili klabu hiyo inakosa uzoefu wa namna ya kudili la usajili tangu Ed Woodward alipomrithi David Gill.
Ed Woodward amefanya kazi nzuri katika upande wa masoko/biashara na anastahili sifa, lakini kazi nyingine pia ni kupata dili zenye kuinufaisha klabu, jambo ambalo amelimudu kwenye biashara za matangazo/udhamini kwa mfano dili za Adidas na Chevrolet. Adidas watailipa Man United €750m kwa miaka 10 na Chevrolet watalipa kiasi cha €350M kwa muda wa miaka 7..
Linapokuja suala la uhamisho wa wachezaji, Woodward bado anaonekana kutokufanya vizuri – mfano ukiangalia uhamisho aa Maroune Fellaini kutoka Everton kwenda United – Man United walilipq £4m zaidi ya ilivyotakiwa katika kipengele cha kuvunja mkataba wa Fellaini na Toffes na pia alifeli katika usajili wa Pedro kutoka Barcelona baada ya kuzidiwa kasi na Chelsea. United pia walimsajili Anthony Martial kwa £36m na inaweza kufika zaidi ya £50m ikiwa atapata mafanikio na klabu hiyo, hili liliwafanya watu/wachambuzi wa soka kuanza kuwa na mashaka na utendaji wa United kwenye suala la uhamisho wa wachezaji na je kama wana mipango endelevu ya mbeleni.
Tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu, Man United wamekuwa katika kipindi cha mpito wa mabadiliko na kipindi hiki kitaendelea mpaka Louis Van Gaal atakapoondoka mkataba wake utakapoisha 2017. Louis Van Gaal kwasasa hasumbuliwi na mafanikio ya muda mfupi, naamini maono yake yanatoa majawabu endelevu ya kipindi cha mbele na anatengeneza msingi mzuri kwa kocha ajaye wa Manchester United.
WACHEZAJI WALIOUZWA NA UNITED CHINI YA LVG
Sera ya Louis Van Gaal katika kuijenga United itakayodumu kwa kipindi kirefu inaweza kuonekana katika madirisha mawili ya usajili ya mwaka 2014 na 2015. Wakati vipindi hivi viwili vya usajili – Van Gaal amewauza wachezaji wa kikosi cha kwanza 13 ambao umri wao ulikuwa si chini ya miaka 27 na wachezaji wengine ambao hawakuwa wanafiti kuendelea kuitumikia klabu, wachezaji aina ya akina Nani, Anderson, Welbeck, Cleverley, Evans na hata Angel Di Maria (aliyetaka kuondoka mwenyewe). Kama Louis Van Gaal angewaacha wachezaji hawa klabuni basi wangeuzwa msimu ujao au wa baada hivyo uamuzi wa kuwauza ndani ya miaka vipindi viwili vilivyopita vya usajili ulikuwa sahihi kwa sababu United imewauza wakiwa bado na thamani katika soko la usajili. Kama angewaacha wangeendelea kuwa mzigo wa ziaa usioendana na mahitaji ya timu kwa kocha ajaye – na labda isingepatikana wigo mpana wa kusajili wa wachezaji wapya.

Filed Under:
EPL,
INTERNATIONAL NEWS,
SPORTS,
TRANSFERS
on Tuesday, September 29, 2015
Post a Comment