KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Jerry Muro afisa habari wa klabu ya Yanga wakati akiongea na waandishi wa habari
Baada ya Yanga jana kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa, afisa habari wa klabu ya hiyo Jerry Muro leo amemtupia kijembe mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Hans Poppe kwa kusema tangu sasa atakuwa akiitwa Hans Pole na si Hans Poppe kama ilivyozoeleka.
Muro ameto kijembe hicho leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya Yanga mtaa wa Jangwani.
“Tulisikia wenzetu wametuandalia supu ya mawe na kachumbari ya miiba, mimi nadhani sasa ufike wakati wa kufungua macho na kuangalia, jana Mkwasa alisema ile supu waliyotuandalia walionja wao kwanza ikawamaliza”, amekejeli Muro.
“Kwahiyo kwa mzee wangu mimi nimpe pole na sisi kwetu tangu jana tunamwita Hans Pole sio Hans Poppe. Najua anaumia ila mimi siwezi kumjibu kwasababu ni mtu mzima sawa na baba yangu amenizidi umri”.
“Namuombea Mungu aishi miaka mingi ili aone tunachokifanya, nadhani sasahivi sukari na presha viko juu ila sisi tunampa pole akae sawasawa ajipange na ajichunguze”
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment