IVO MAPUNDA ASHINDWA KUJIZUIA JUU YA NYOSSO, HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK…

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Ivo Mapunda 1
Kipa wa zamani wa klabu za Tanzania Prisons, Moro United, Yanga SC, St.George ya Ethiopia, African Lyon, Bandari FC na  Gor Mahia FC za Kenya, Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Ivo Mapunda amelaani vikali tabia ya Jums Nyosso kuwadhalilisha wachezaji wenzake kwa kuwashika sehemu za makalio.
“Binafsi nachukua nafasi hii kuwaomba wachezaji wenzangu, wanaocheza na waliowahi kucheza soka, wadau wote pamoja na mashabiki wa ndani na nje ya nchi KULAANI kwa nguvu zote tabia na vitendo vya aibu na udhalilishaji anavyofanya mchezaji mwenzetu Nyosso” ameandika Ivo katika akaunti yake ya facebook mchana huu.
“Hii ni aibu, siyo yake pekee bali ni yetu sote wachezaji hasa wa medani ya kimataifa. Tunaonekana ‘hopeless’ pia na hata kukosa nafasi ya kwenda nje ya kucheza soka kutokana na tabia dhalimu. Tunaomba adhabu yake itakayotolewa iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hii. Wanajifunza nini watoto au vijana wanaochipukia katika soka kwa huu udhalilishaji ukizingatia Nyosso ni mchezaji mkubwa?”
Ivo Mapunda
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top