Siku mbili baada ya kufunga goli lake la kwanza katika Barclays Premier League, winga wa Manchester United Memphis Depay aliamua kujipongeza kwa kwenda kufanya shopping huko Selfridges jijini Manchester huku pembeni akiwa na kampani ya demu wa zamani wa mwanamuziki Chris Brown – Kerrueche Tran.
Wawili hao Depay, 21, na Kerrueche walionekana pamoja tena jumamosi iliyopita usiku wakiwa katika klabu ya Club LIV.
Wawili hao walianza kuwa na ukaribu na kuonekana pamoja wakati Depay alipoenda nchini Marekani kwa mapumziko siku chache baada ya kujiunga na Manchester United akitokea PSV Eindhoven.
Mpaka sasa haijathibitishwa aina ya urafiki walionao wawili hao japo tetesi zinasema wanashea kitanda.
Depay mpaka sasa ameshaichezea United mechi 11 na kufunga magoli 4, goli lake la kwanza kwenye EPL limeisadia United kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza tangu utawala wa Sir Alex Ferguson
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment