MAN U YANATAMBULISHA UZI ULOVUNJA REKODI YA MKWANJA DUNIANI

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
 Manchester Kit
Manchester United imekuwa miongoni mwa klabu ambazo zimetambulisha jei zao zitakazotumiwa kwa ajili ya msimu ujao. Klabu hiyo imevunja rekodi kwa kuwa ni klabu inayopiga pesa nyingi duniani kutoka kwa watengezaji wa jezi ambapo jezi zao zitakuwa zikitengenezwa na kampuni ya Adidas baada ya kusaini dili la pauni milioni 750.
Kabla ya Adidas Nike ndio walikuwa watengenezaji wa jezi za mashetani wekundu na wamedumu kwa muda wa miaka 13 kabla ya Adidas kuchukua dili hilo baada ya mkataba wa Nike na Man U kumalizika.
Wakongwe hao (Adidas) wa kutengeneza vifaa vya michezo wanaamini wnaweza kutengeneza kiasi cha pauni bilioni 1.5 kutokana na mauzo ya jezi za Man U kwa muda wa miaka 10 ijayo.
Dili hilo kati ya Manchester United na Adidas linayapiku madili mengine ya klabu ambazo zinatengenezewa jezi na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na klabu Bayern Munich (pauni milioni 645) na Chelsea (pauni milioni 300).
Jezi hizo mpya zitakuwa na muonekano kama ule wa zamani enzi za Ryan Giggs zikiwa na shingo ya V yenye rangi nyeupe na michirizi mitatu kwenye mikono yake.
Manchester Kit 1
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top