BREAKING NEWS: TATU BORA YA KING'ANYIRO CHA UENYEKITI CCM IMETANGAZWA ( MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM)

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Katika kile ambacho wengi hawakutarajia wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi, umefika katika hatua ya tatu bora baada ya msululu wa wagombea 40 kupunguzwa hadi kufikia wagombea watano na hatimaye kufikia hadi watatu.

Katika nafasi hiyo wagombea wa kike waonekana kutakata baada ya wanawake wawili kufika hatua hiyo; katika nafasi hiyo Mheshimiwa Bernard Membe na Mheshimiwa January Makamba walijikuta wakiishia nafasi ya tano bora na kuwapisha wengine watatu wakisonga mbele.
wagombea watatu hao ni kama unavyoyaona katika picha iliyo kushoto kwako.

Tazama wasifu wa wagombea hao kwa ufupi:

1. ASHA-ROSE MIGIRO

Asha-Rose Migiro, mmoja wa wagombea watano ni mbunge wa kuteuliwa katika bunge, na waziri wa sheria na katiba Tanzania.


Mhe. Migiro amesomea sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na shahada ya uzamivu yake katika chuo cha Konstanz (Ujerumani). Kabla ya kujiunga na siasa, alikua mhadhiri mkuu wa mafunzo ya sheria Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam. Pia aliwahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007-2012)

2. AMINA S. ALI



Mfahamu Amina Salum Ali, mmoja wa wagombea watano. Aliwahi kuwa waziri wa Fedha (Zanzibar; 1990-2000), na ni balozi wa Umoja wa Mataifa ya Afrika nchini Marekani (2007-2015). Amesomea uchumi katika chuo cha Delhi na pia ana MBA ya Masoko kutoka chuo cha Pune.

3. JOHN POMBE MAGUFURI

Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29,1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  • Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza. 
  • Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. 
  • Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. 
  • Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa. 
  • Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. 
  • Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera. 
  • Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.
Mafunzo
  • Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
  • Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
  • Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
  • Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
  • Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
  • Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)
  • Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
  • Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
  • Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.
  • Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.

Nyawaye Maswe Gesirali's photo.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top