Mashabiki wengi wa Arsenal hawafurahishwi na kitendo cha kocha wao Arsene Wenger kutulia kipindi hiki cha usajili wakati wanaamini kwamba Mfaransa huyo anatakiwa kutafuta mshambuliaji mmoja wa kati. “A central Striker”.
Wakiwa wamemsaini Petr Cech ambaye tayari ameonesha ubora wake, mashabiki wa Arsenal wanajiamini kwamba Francis Coquelin na Santi Cazorla ni viungo wanaoweza kuwapa ubingwa.
Aaron Ramsey na Jack Wilshere pia ni viungo wa kati wanaotosha kuipa Arsenal mafanikio, lakini safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Olivier Giroud na Theo Walcott haiwezi kutimiza ndoto zao.
Kiukweli Giroud alipata wakati mgumu msimu wa 2014/2015 na sasa mashabiki wanasikia tetesi kuwa klabu yao inataka kumsajili Karim Benzema na Gonzalo Higuain, lakini Wenger amekanusha.
Siku za karibuni Higuain amechemsha sana na inamaanisha Wenger anatupia macho kwa Benzema ambaye bado anahitajika Real Madrid.
Giroud atafurahia kuondolewa katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal?
Mfaransa huyo amezungumzia hali hiyo hapa chini:
“Sifikirii swali hili kiukweli. Najaribu kuangalia zaidi maandalizi yangu ya msimu mpya. Tunafanya vizuri sana kama timu, kitu cha msingi siku zote kwangu ni kuona timu inaimarika, najitahidi siku zote kujitolea kadri niwezavyo. Kama atakuwepo straika mwingine, itakuwa vizuri kwa timu nzima kwasababu ushindani ni mzuri kwa kila mtu”.

Post a Comment