Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Zacharia Hans Poppe ametishia kuacha kutumia bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya Azam, hii ni kutokana na kuondokewa na kijna wao Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyejiunga na kikosi cha Azam FC ‘Wanalambalamba’ kwa mkataba wa miaka miwili.
Poppe amesema, pesa wanazopata Azam kutoka kwenye bidhaa zao ndizo zinazotumika kufanya ‘udhalimu’ na kumlipa mshahara moja ya kiongozi wao Saad Kawemba ili atekeleze mambo hayo.
“Mimi nahasira na Azam nataka kuanzia sasa hata maji ya Azam sitaki kunywa, bidhaa zao zote sijui keki, ice cream sitaki, kwasababu hiyo hela wanayopata pale ndio wanakuja kutumia kwenye udhalimu huu na yeye Kawemba wanamlipa mshahara aje afanye mambo kama haya”, amesema Poppe.
“Sasa labda tupunguze kipato chao twende katika mambo kama haya?”, alihoji.
Azam wamekuwa wakishutumiwa kuwa, walikuwa wakichochea kuvunjwa kwa mkataba kati ya Simba SC na Ramadhani Singano ili wao (Azam FC) wamsajili mchezaji huyo kama mchezaji huru.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment