Kafulila atakiwa Kulipa Milioni 7.5 Kama Dhamana Ya Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) kwa miaka mitano iliyopita, David Kafulila ameamriwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora kulipa Sh7.5 milioni kama dhamana, ili ombi lake lakutaka itengue matokeo ya ubunge wa jimbo hilo yasikilizwe.

Mahakama imetoa uamuzi huo kupitia kwa Jaji Leiyla Mgonya, baada ya kuzingatia maombi ya Kafulila aliyetaka apunguziwe gharama  ya fedha za dhamana kutoka Sh5 milioni badala yake alipe Sh1 milioni kwa kila mdaiwa.

Kupitia Wakili wake, Emmanuel Msyani, Kafulila aliwasilisha ombi Mahakama Kuu alipe Sh1 milioni kama dhamana kwa kila mlalamikiwa kwa kuwa hana uwezo wa kulipa Sh15 milioni zilizotajwa kwa mujibu wa sheria ya kesi za uchaguzi kwa mtu anayepinga matokeo.

 Baada ya uamuzi huo kutolewa, alisema anakubaliana nao na yupo tayari kulipa kiasi hicho cha fedha ili kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani iweze kusikilizwa na kutolewa hukumu.

 Katika maombi yaliyowasilishwa na Wakili Msyani kwa niaba ya Wakili Daniel Lunyemela ambaye hakuwapo mahakamani, aliiomba Mahakama ikubali  ombi la  mteja wake kwamba, hataweza kumudu kulipa kiasi kilichokuwa kikitakiwa cha Sh15 milioni.

 Msyani aliiambia Mahakama kuwa kutompunguzia gharama mteja wake ni kumnyima haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika chombo cha sheria kama ilivyoainishwa.

Upande wa utetezi uliowakilishwa na mawakili  waandamizi wa Serikali,  Juma Masanja na Kennedy Fungamtama, waliiomba Mahakama itupilie mbali maombi hayo kwa madai kuwa Kafulila ana mali na fedha ambazo alilipwa zaidi ya Sh200 milioni na kwamba, alikuwa akilipwa na Bunge kila mwezi Sh11 milioni

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top