Magufuli Aitaka TRA Kutoa Mashine za EFDs Bure.

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameishangaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kutogawa bure Mashine za EFDs, na wao kubaki na kazi ya kukusanya mapato.

Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji jana jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), alisema muda uliopotea na kodi ambayo haikukusanywa wakati wa mvutano na wafanyabiashara ungetosha kununua mashine mpya na kuwagawia.

“Kama mnajua mashine hizi ni halali na ni zenu, wapeni bure kazi yenu iwe ni kukusanya kodi, ni hesabu rahisi sana isiyohitaji kwenda chuo kikuu kuwa muda uliopotea na fedha hazifiki bilioni 12 zingetosha kununua na iwe kazi ni kukusanya kodi,” alisema.

Awali katika salamu zake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Jonson Minja, alimpongeza rais kwa kazi kubwa aliyofanya Bandarini na TRA kwa kuwa imewezesha kodi kukusanywa kwa usahihi na kwamba kipindi cha nyuma fedha nyingi zilipotea, kutokana na mfumo wa ukusanyaji kodi kutowekwa wazi.

Aidha, alisema mashine za EFDs zitatumika kwa wafanyabiashara wote mwakani, kwa kuwa changamoto zilizosababisha mvutano baina yao na serikali zimemalizika.

Aidha, alimtaka rais kufuatilia kwa karibu ukwepaji kodi katika sekta isiyo rasmi na kwamba kukiwa na mipango madhubuti serikali itaweza kupata kodi kwa wananchi wote.

“Kasi ya rais inatupa matumaini makubwa sana, tunachoweza kusema, Mungu akubariki akupe hekima na nguvu...tunaomba uimarishe viwanda vya kati na vidogo ili malighafi zisisafirishwe kwenda nje, bidhaa ambazo zitasaidia kukuza uchumi na kuimarisha shilingi dhidi ya Dola ya Marekani,” alisema.

Tangu mwaka juzi kulikuwa na mvutano mkali baina ya wafanyabiashara na TRA, ambao waligoma kutumia mashine hizo hadi serikali itakaposhughulikia kero zao ikiwamo bei ya mashine, utitiri wa kodi, ukwepaji kodi na urasimu uliopo.

Wafanyabiashara kwa umoja wao waliitisha mgomo nchi nzima na kumekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na serikali, ambayo wakati mwingine hayakufikia ukingoni, hatua iliyofanya baadhi ya viongozi wa wafanyabiashra kukamatwa.

Minja alikamatwa na Polisi mkoani Dodoma mwaka jana, na kuswekwa ndani, jambo lililofanya wafanyabiashara kuitisha mgomo wa siku tatu hadi serikali itakapoeleza alipo kiongozi wao.

Baadaye ilibainika anashikiliwa na Polisi mkoani humo, na alipandishwa mahakama ya mkoa na kusomewa mashtaka ya kuchochea mgomo wa wafanyabiashara nchini.

Baadaye mahakama ya mkoa ilimuachia huru kiongozi huyo.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top