WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Jana ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
"Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.
Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, NOVEMBA 23, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia ofisini kwake , Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha kwa watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post a Comment