Lowassa Awatembelea Wahanga Waliookolewa Mgodini Baada ya Kufukiwa Kifusi Kwa Siku 41

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;


Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa Jana alitoa shilingimilioni mbili kwa wahanga waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.

Akikabidhi fedha hizo kwa wahanga hao, Lowassa alisema ametoa fedha hizo kama msaada ili ziwasaidie kwa matibabu kwa muda wote watakapokuwa hospitalini hapo, ambapo kila mmoja amepatiwa shilingi laki tano.

Mmoja wa wahanga hao, Joseph Burule alisema kitendo cha Lowassa kuwatembelea hospitalini hapo kimewapa faraja kubwa, kwani tangu waokolewe na kuanza kupatiwa matibabu hakuna kiongozi mkubwa aliyefika kuwajulia hali pamoja na kuwapa pole.

Burule alisema kitendo hicho kinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi pindi linapotokea jambo la kusikitisha kama hilo, na kusema kuwa fedha hizo zitawasaidia kujikimu hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA Salome Makamba aliwaambia wananchi waliojitoza kumsabahi Lowassa kuwa, Lowassa amekuja kuwapa pole wahanga hao na hakuja kwa masuala ya kisiasa.

Novemba 15, 2015 wahanga 5 kati ya 6 waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya nyangalata wilayani kahama waliokolewa wakiwa hai baada ya kukaa ndani ya mashimo kwa siku 41, ambapo juzimmoja kati yao alifariki dunia.

Ni hivi karibuni baada ya kuokolewa mmoja wa wahanga hao alikaririwa akimuulizia Lowassa kama alishinda urais wa  Tanzania kwenye uchaguzi na baada ya kuambiwa hakushinda alikosa raha.


KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top