Kafulia Afungua Kesi Mahakama Kuu Kupinga Ushindi wa CCM.......Tundu Lissu Ajitosa Kumtetea

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR -Mageuzi, David Kafulila, amewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kupinga ushindi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasna Mwilima.

Akizungumza na mtandao huu jana baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Kafulila alisema amefungua kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015 ya uchaguzi, akiwalalamikia Mwilima, msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Alisema kesi hiyo itasimamiwa na mawakili wawili, Tundu Lissu na Daniel Lumengela, huku hoja ya msingi katika shauri ikiwa ni kupinga matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi ambayo anadai si halali kwani kutokana na fomu 382 za vituoni na kusainiwa na wasimamizi na mawakala, alipata kura zaidi ya 34,000 dhidi ya 32,000 za mpinzani wake (Mwilima).
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top