Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama za serikali/umma, kwa mwaka huu.
Balozi Sefue, ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.
Badala yake Balozi Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
26 Novemba, 2015
Post a Comment