Lissu alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani humo ambapo alibainisha kuwa amepata taarifa kupitia njia ya simu kutoka kwa meneja wa mkoa wa benki moja mjini hapa na askari polisi wawili, kwamba jeshi la polisi limeandaa nguvu kubwa kupindua maamuzi ya wapiga kura, ili mgombea wa CCM atangazwe mshindi
Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, alisema kwa nyakati tofauti, alipigiwa simu na askari polisi wawili akiwemo wa FFU, na kumpa taarifa ile ile aliyopewa na meneja wa benki.
Mgombea huyo alisema kwa akili ya kawaida, jeshi la polisi halipaswi kutuma nguvu kubwa jimbo la Singida mashariki ambalo toka kampeni zianze, hapajatokea tukio au dalili za uvunjivu wa amani.
Katika hatua nyingine, Tundu Lissu ameahidi kwamba endapo atashindwa kihalali, atakubaliana na matokeo na hatakuwa na kinyongo chochote.Lakini endapo atashindwa kwa mbinu chafu, hatakubaliana na matokeo hayo machafu.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sedoyeka, alisema wamemtaka Lissu kwa kuwa ni mwanasheria, athibitishe tuhuma zake hizo, ndipo jeshi la polisi liweze kuchukua hatua stahiki.
Katika jimbo hilo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemsimamisha Bw.Jonathan Njau kupambana na Tundu Lissu katika uchaguzi huu. KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment