MOSHI MABOMU YARINDIMA KWENYE MKUTANO WA MGOMBEA WA CCM, POLISI WANAFANYA KAZI KUTULIZA VURUGU ILA VIJANA WAMECHACHAMAA

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Moshi. Vijana 50 wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema, wanadaiwa kufanya fujo kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea wa ubunge wa CCM katika Jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha na kusababisha polisi wawatawanye kwa mabomu ya machozi.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Rau Madukani, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema mgombea wa CCM akiwa anatarajia kuzungumza na wanachi katika eneo hilo, kulitokea kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia 50 wakiwa na silaha za jadi, marungu, mawe na fimbo na kuanza kuwashambulia watu waliokuwa katika mkutano wa mgombea huyo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema katika Manispaa ya Moshi, Jafari Michael ambaye pia ni mgombea ubunge, alikanusha vijana wa Chadema kufanya vurugu hizo, bali alidai zilifanywa na vijana ambao hawajulikani wana itikadi ya vyama gani.
Michael alivilaumu vyombo vya dola kuwa vinawapendelea CCM kiasi cha kila jambo likifanyika huwatuhumu vijana wa Chadema.
“Hata tukipeleka malalamiko polisi hawatusikilizi na hata kama vurugu zikifanywa na wafuasi wa CCM wanasema ni Chadema, wanatuonea sana hawa jamaa,” alilalamika Michael.
Alisema vijana waliokamatwa mtu hawezi kuwatuhumu moja kwa moja kuwa ni wa Chadema, kwa kuwa hawajulikani itikadi zao.
Kamanda Ngonyaji alidai kuwa chanzo cha vurugu hizo ni baada ya wafuasi wa CCM kudaiwa kushusha bendera za Chadema zilizokuwa zimesimikwa uwanjani hapo.
Alisema vurugu hizo zilisababisha majeruhi wawili aliowataja kuwa Wilson Fabian (23) aliyepigwa jiwe kwenye paji la uso pamoja na mkono wa kulia, mwingine hakufahamika jina mara moja na wote walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.
Ngonyani alidai kuwa vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa magari yaliyokuwapo uwanjani hapo baada ya kuvunjwa vioo.
Alisema watu kumi na moja wanashikiliwa kwa mahojiano kutokana na vurugu hizo kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top