KAULI YA " LAZIMA TUSHINDE" YAZUA MAKUBWA HUKO MAKETE NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MKUU AFANYA MAAJABU KWA WANANCHI HUKO MAKETE

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Kutokana na baadhi ya watu kutoaana umuhimu wa kipiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa sababu mbalimbali ambazo zinaweza kuepukika, shirika la SHICODA lililopo mkoani Njombe limetoa elimu kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali wilayani Makete mkoani hapo ili waweze kuwahamasisha watu kupiga kura mwaka huu

Mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Spiritual Centre Makete mjini, yamehudhuriwa na wawakilishi wa makundi mbalimbali hasa yasiyopewa vipaumbele lakini yana umuhimu kwa jamii amabyo ni walemavu, vijana na wanawake

Akifungua mafunzo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Francis Namaumbo amesema washiriki hao wanatakiwa kutoa elimu wanayoipata kwa wale waliopo kwenye maeneo wanayotoka, hasa ukizingatia zipo kauli zinazotolewa na baadhi ya wagombea ambazo zinaonekana kutisha wananchi na wakaogopa kwenda kupiga kura

Namaumbo ametolea mfano wa kauli ya 'Lazima Tushinde" kwa kudai kuwa ni kauli inayoonekana kutisha watu na wanasahau kuwa katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa hivyo unapoweka neno lazima kutasababisha ugumu wa kupokea matokeo hasa kwa wale walioshindwa

Amewataka washiriki hao pia kuwapa elimu wale waliowaacha huko watokako namna ya kukubali kupokea matokeo kwa upande wanaoushabikia hasa ikizingatiwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi, hivyo kama kila mmoja atataka awe mshindi ha hatakubali kukubaliana na matokeo hali ya maelewano haitakuwepo

Afisa Mtendaji mkuu wa shirika la SHICODA Bw. Aloyce Msigwa amesema wameamua kuandaa mafunzo hayo katika wilaya ya Makete kutokana na kuwepo makundi ambayo waliyalenga, na kusema wamelenga kata 17 za wilaya hiyo zitanufaika na mafunzo hayo

Amesema pia wanaendesha mafunzo hayo pia katika kata kadhaa za wilaya ya Njombe na wilaya ya Wangong'ombe

Baadhi wa washiriki waliozungumza na eddy blog ni Bi Maurisia Sanga na Nebert Sigalla ambao wamesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo kwa pamoja wamesema watakwenda kufikisha elimu waliyoipata na kudai kuwa watu wanatakiwa kuanza kufanya maandalizi sasa hivi, ikiwemo kuandaa kadi zao za kupigia kura, pamoja na kwenda kuhakiki majina yao kwenye vituo walivyojiandikishia..

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top