HABARI YA HIVI PUNDE:..MGOMBEA URAIS WA ACT-WAZALENDO AMFANYIA KITU MBAYA DR. MAGUFULI NA HILI HALIJAWAHI KUTOKEA MIAKA YOTE

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;


Watanzania wametakiwa kutomchagua mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kwa madai kuwa Serikali iliyopo madarakani inatumia mabilioni ya fedha kununua fulana, kofia na kugawa bure, huku ikishindwa kuwalipia chakula wanafunzi shuleni. 

Wito huo ulitolewa jana na mgombea urais wa ACT ­Wazalendo, Anna Mghwira kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Mbuzi uliopo mji wa Mugumu wilayani hapa Mkoa wa Mara. 

Mghwira (pichani) alisema mfumo mbovu wa CCM na Serikali yake, umechangia huduma za jamii kuuzwa na wanafunzi kukosa chakula shuleni. 

Huku akishangiliwa na umati uliofurika kusikiliza sera za ACT Wazalendo, licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha, Mghwira alisema ni kipindi cha kuikataa CCM kwa kuwa haina uchungu na wananchi, badala yake imekuwa ikiwakumbuka wakati wa uchaguzi kwa kuwapatia fulana na kofia bure.

“Sasa hivi tisheti za njano na kofia zimetapakaa sana, wanagawa bure na kusomba watu kwa malori ili wajae kwenye mikutano yao, wakati watoto wanakaa chini, hawapati chakula shuleni, watumishi hawalipwi, dawa hospitali hakuna, barabara mbovu. 

Ni kipindi cha kuwataka wapishe Ikulu,” alisema. 

Kuhusu kauli za Magufuli kwamba Serikali yake itakuwa ya viwanda, alisema anatakiwa kuwatajia Watanzania aliyeviuza viwanda 300 vilivyojengwa Mwalimu Nyerere wakati wa uongozi wake. 

Kuhusu ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, alidai kauli anazotoa mgombea huyo wa CCM hazina ukweli kwa sababu barabara ya kutoka Bunda hadi Serengeti haifai kutoka na ubovu. 

“Kwa zaidi ya miaka 15 wanawaahidi tu, wilaya hii yenye neema na jina kubwa ndiyo imesahaulika hivi, wanathamini wanyama kuliko watu. Muikatae CCM mwaka huu,” alisema.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top