KAMPENI za wagombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini zimesimama kufuatia kifo cha Mgombea Ubunge wa chama cha ACT-Wazalendo, Estomiah Mallah aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC iliyopo wilaya ya Moshi, Kilimanjaro, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu.
Akithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Mgombea huyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd ambaye pia ni Msimamizi mkuu wa Uchaguzi katika jimbo hilo, Idd amesema kuwa kampeni ambazo zitaendelea ni za urais na udiwani, lakini wabunge mpaka tume ya uchaguzi ipange upya ratiba.
“Kweli mgombea amefariki na nimepata taarifa za kifo hiki leo saa 12:00 asubuhi, toka kwa katibu wa chama chake marehemu ACT-Wazalendo, Eliamam Motivo,” amesema.
Aidha ametoa pole kwa wafuasi wa chama hicho kwa kuondokewa na mpendwa wao na wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu.
Katibu wa Jimbo la Arusha wa Chama cha ACT-Wazalendo, Eliamam Motivo amesema amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa mgombea wao na Mshauri Mkuu wa Chama chao kwa mkoa wa Arusha.
“Mzee alikuwa haumwi lakini kwenye mkutano wa mgombea urais wa chama chetu Oktoba 6, alipanda jukwaani na baada yakushuka alisema hajisikii vizuri na kesho yake ambayo Oktoba 7 alikwenda hospitali ya St. Thomas na alipatiwa matibabu ila hali yake iliendelea kuwa mbaya na tuliamua kumwamishia hospitali ya KCMC na usiku wa kuamkia leo saa saba usiku alifariki,” amesema.
Motivo alisema chama hicho kimesimamisha kampeni zote, kwa siku tatu ili kuomboleza msiba huo.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment