MAMBO YA KUVUTIA YALIYOJIRI KWENYE USIKU WA UEFA WIKI HII.>>>>>> SOMA HAPA

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

UEFA Champions League ratiba

Na Salym Juma
Nikiamini hali zenu ni njema, karibuni sana katika ukurasa huu ili kuweza kupata habari za kipekee ambazo pengine huwezi kuzipata sehemu zingine. Binafsi mimi ni mzima na hata nilisikitishwa na ajali aliyoipata Luke Shaw pale Uholanzi. Pia ushindi wa Mourinho niliutazama kwa macho yangu mawili mchezo wa pale Darajani. Mwenyezi Mungu pia alinipa uzima wa kushuhudia vipigo kwa vilabu vya jiji la Manchester na ile timu moja ya pale London. Kutokana na kujaaliwa pumzi na afya njema hadi kutazama mafuriko ya pale Chato na Kigoma bila ajizi napaswa kusema ‘Al-hamdulillah’ nikiwa na maana ya Mwenyezi Mungu asante.
Leo hii nimejaaliwa kukuletea matukio ambayo yamejiri na kuweka rekodi kwenye usiku wa UEFA kwa timu, Makocha na Wachezaji mbalimbali. Ungana nami hapa chini kufahamu mengi kuhusu usiku wa UEFA uliomalizika siku ya Jumatano.
Mchawi wa soka duniani, Lionel Messi baada ya kushindwa kuifunga As Roma kwenye usiku wa UEFA, hatimaye amekamilisha mechi 3 mfululizo za UEFA bila kufunga goli wala kutoa assist. Huu ni ukame ambao haukuwahi kutokea tangu September 2008.
Baada ya juzi Cristiano Ronaldo kufunga penati 2, hatimaye Mshambuliaji huyo amekuwa ndiye Mchezaji aliyefunga penati nyingi zaidi kwenye michuano hiyo. Hadi sasa jamaa amefunga mikwaju 11 ya enati kwenye UEFA.
Baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Dinamo Zagreb, Meneja wa Arsenal, Mzee Arsenal Wenger amekuwa Meneja wa kwanza kupoteza kwenye mechi yake ya 50 ya mashindano. Wenger alifungwa ugenini baada ya timu yake kucheza pungufu kwani Giroud alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Baada ya Man United, Arsenal na Man City kupata vipigo kwenye usiku wa UEFA, hii ni mara ya kwanza kwa timu 3 za Uingereza kupoteza michezo yao ya ufunguzi huku timu zote zikipoteza kwa magoli 2-1. Chelsea ndiyo timu pekee ya Uingereza iliyopata ushindi tena wa kishindo.
Dinamo Zagreb haijawahi kufungwa ndani ya miezi 11 huku ikiwa imecheza michezo 42. Ushindi wa kwenye UEFA dhidi ya Arsenal ulikuwa ni mwendelezo wa timu hii ambayo imetoa Mastaa kibao wanaotikisa bara la Ulaya kwa sasa akiwemo Luca Modric na Mario Mandukisc.
Baada ya Diego Costa kuwafunga Wayahudi kwenye usiku wa UEFA, unapaswa kuamini kuwa lile ndiyo lilikuwa goli lake la kwanza kwenye UEFA tangu April 2014 alipowafunga Chelsea kwa penati akiwa Atletco Madrid. Costa pia alisababisha penati kwenye usiku wa jana.
Japokuwa Lionel Messi hakufunga kwenye usiku wa UEFA ila alifanikiwa kuwa mchezaji mdogo kucheza mechi ya 100 ya UEFA akiwa na miaka 28 na siku 84. Raul ndiye alikuwa mmiliki wa rekodi hii hapo awali kabla ya usiku wa jana.
Francis Coquelin ndiye mchezaji pekee katika vilabu 4 vya EPL  vilivyocheza kwenye UEFA wiki hii aliyeingia uwanjani huku akiwa anaongoza kufanya ‘tackles’ kwa kuwa na wastani wa ‘tackle’ 4.4 kwa mechi moja. Hii ina maana alitegemewa kupunguza mashambulizi na kuharibu mipango ya adui licha ya kutocheza dakika zote.
Thomas Muller alifunga magoli 2 kwenye usiku wa UEFA na hatimaye kuweka rekodi kwenye klabu na timu yake ya taifa kwa kufunga magoli 11 katika mechi 7. Unaweza ukaona ni rekodi ya kawaida ila hakuna mtu aliyefanya hivi karibuni pale Ujerumani. Kitendo hiki ni kawaida sana kwa watu kama akina Neymar, Messi na Ronaldo.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top