KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Katibu mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, Jerome Valcke amesimamishwa kuendelea na majukumu yake ili kupisha uchunguzi wa kamati ya maadili ya FIFA kuchunguza kwa uhakika suala linalomkabili.
Jerome Valcke anakabiliwa na skendo ya uuzaji tiketi za kombe la dunia kwa magendo. Mfaransa huyo ambaye aliingia madarakani tangu mwaka 2007 hivi sasa atafanyiwa mahojiano na polisi wa Zurich na kamati ya maadili ya FIFA.
FIFA chini ya rais aliyejiuzulu Sepp Blatter ipo katika kashifa nzito za rushwa tangu mwezi Mei mwaka huu, huku maafisa usalama wa Marekani wakiwashikilia maafisa saba wa shirikisho hilo kwa tuhuma za rushwa.
Jerome Valcke ambaye ni namba 2 wa Sepp Blatter alitarajiwa kusimama kama rais wa shirikisho hilo baada ya Blatter kuondoka, lakini hivi sasa yuko kikaangoni kwa mahojiano zaidi.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment