Kwenye stori ya Hekaheka leo ni ya JB kuhusu utapeli, amesema wakati akiwa nyumbani hana kazi baada ya kumaliza masomo yake, anasema alipewa jukumu la kuangalia kuku na kuuza, siku moja akaja mteja anataka kuku , na alisema yupo tayari kuchukua kuku wote 600.
Kabla ya dk5 kuisha ikaja gari kupakia kuku, anasema kuku wote wakawekwa kweye gari, wakati anaomba hela yake baada ya kumaliza kupakia akaambiwa atapewa baada ya kufikisha kuku wote sehemu husika maeneo ya Temeke.
Baada ya kuwashusha, akamuaga kuwa anaingia ndani wakati yeye anamsubiri nje, alikaa muda mrefu bila kumuona na kuamua kuingia ndani lakini hakumkuta.
Msikilize hapa akizungumza kwenye Hekaheka…
Post a Comment