BAADA YA TWAWEZA KUSEMA CCM INAKUBALIKA 66% HAYA NI MANENO 15 YA LOWASSA NA 26 YA ZITTO KABWE

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%C.U.F 1%,ACT 0%NCCR 0%UKAWA 3%.
Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo.
Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter >>> ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata
Dr. Magufuli hakuwa ameandika chochote kuhusu utafiti huu huku tweet yake ya mwisho ikiwa inaeleza furaha yake kwa jinsi Wananchi wa Bukoba walivyojitokeza kumsikiliza.
Kwa upande wa ACT Wazalendo, kiongozi wake Zitto Kabwe aliandika kwenye Twitter ‘Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura’
Kingine alichosema Zitto ni >>> ‘Ikumbukwe kwamba utafiti huu wa TWAWEZA umefanywa kabla ya chama cha ACT WAZALENDO hakijapata mgombea Urais na kabla ya uzinduzi vilevile
January Makamba wa CCM kwenye sehemu ya Tweets zake aliandika kwamba hajashangazwa na matokeo ya utafiti wa TWAWEZA sababu imeendana na utafiti na CCM ambao ulitangazwa siku chache kabla.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top