Kuna sababu ya Ccm kuwasikiliza ahadi zao tena......
Twende Pamoja tukumbuke chaguzi zilizopita
----------------------------------------
Ahadi za JK kwenye kampeni za urais 2010
============================
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5. Kumaliza migogoro yote ya Ardhi nchini- Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma
36. Kulinda haki za walemavu- Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa
57. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kibandamaiti mjini Zanzibar
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbamba bay-Ruvuma
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbamba bay Ruvuma
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha
66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
67. Anawafahamu wauza unga wote Tanzania na atawashughulikia ndani ya siku 100 - Ukonga.
-----------------------------------------
Hapa wala tusiongezee ile ya kuwa na Katiba Mpya kabla hajatoka Ikulu.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment