MAN UTD: KWANINI VAN GAAL BADO ANA KAZI YA KUFANYA…?

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Kocha Louis Van Gaal ametumia zaidi ya pauni 220m katika kipindi cha miezi 14. Tofauti na msimu uliopita Manchester United wakianza vibaya kwa kichapo cha goli 2-1 dhidi ya Swansea, msimu huu wameanza vyema kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur, lakini bado Van Gaal ana kazi ya kufanya.
HIKI NDICHO KIKOSI CHA UNITED HIVI SASA
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23 Manchester United hawajampanga mchezaji angalau mmoja zao la academy. Lakini pia tofauti na kikosi kilichoanza mwaka jana katika mechi ya ufunguzi, wachezaji wanne pekee walianza katika mechi zote mbili, Rooney, Young, Mata na Smalling.
KIKOSI CHA MAN UTD KILICHOCHEZA MCHEZO WA KWANZA DHIDI YA SWANSEA CITY -2014
ma u
Van Gaal aliwachezesha wachezaji wake wapya wote huku akimpa nafasi Ander Herrera na Antonio Valencia kwa kikosi cha mwaka jana.
SAFU YA ULINZI BADO SIYO IMARA
Tofauti na msimu uliopita dhidi ya Swansea, ngome ya United imeonekana iko vizuri zaidi katika mechi hii ya ufunguzi msimu huu. Chriss Smalling ameonekana kukomaa sana huku akitoa hatari zaidi ya mbili golini kwao. Lakini kwa upande wa partner wa Smalling katikati Daley Blind anaonekana kukosa kujiamini na hasa inapokua presha ni kubwa langoni mwake.
Kwa upande wa kipa, Van Gaal anahitaji haraka kutatua sintofahamu ya David De Gea ambaye alimuacha nje kutokana na presha ya mchezaji huyo kutua Real Madrid. Hata hivyo ni mapema kumjaji golikipa aliyepewa nafasi badala yake muagentina, Sergio Romero ingawa alifanya vizuri sana katika mchezo huo.
David De Gea alikua ni nguzo tegemezi katika msimu uliopita na sasa inahitaji kuwa makini na namna ya kuziba pengo lake pindi akiondoka.
FOWADI BADO HAIONESHI MAKALI
Robin Van Persie, Radamel Falcao na Angel Di maria wote wameondoka msimu huu. Katika mechi ya jana dhidi ya Spurs, Memphis Depay, Juan Mata na Ashley Young wote walionekana kuwa vizuri lakini tatizo hapa ni pace ya Mata na Depay kuwa haitoshi kumsapoti Wayne Rooney katika mashambulizi na kutia presha langoni mwa wapinzani.
Ashley pekee alijitahidi kujaribu kama mara tatu lakini United wanamhitaji mchezaji mwingine mwenye pace ‘kasi’ kumsaidia Rooney.
HIKI NI KIKOSI CHA MAN UTD KILICHOCHEZA DHIDI YA TOTENHAM -2015
man u 1
Kwa upande wa Wayne Rooney anacheza vizuri nafasi yake ingawa bado hafanyi vizuri zaidi ya akicheza namba kumi ambapo anakuwa na movements za hatari kumsapoti mshambuliaji. Hata hivyo ishu ni kwa hawa wanaomzunguka kuongeza kasi zaidi.
USAJILI MPYA NA MAAMUZI MAGUMU
Tofauti na msimu wa mwaka jana ambapo Van Gaal alikua hajaijua first eleven yake vizuri, msimu huu ana kazi ya kuwaingiza katika mfumo wa timu yake.
Manchester United wana pesa za kutosha kusajili mchezaji yeyote, na kwamba wataweza kumuuza ama kumnunua yeyote ili kugombania tena ubingwa wakiouchukua tangu mara ya mwisho 2013.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top