Mkorogo wangu unawahusu nini?- Linah Sanga
Msanii wa bongo fleva Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi hisia zake za wazi juu ya watu ambao wanamsema vibaya kutokana na mabadiliko yake hususani ya rangi, na kuhisi kuwa huenda ameanza kujichubua jambo ambalo linaonyesha mashabiki wake wamekuwa
wakimsema na kumtupia maneno ya kejeli. Linah kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema amechoka na maneno na kufuru za mashabiki juu ya maisha yake na kuwataka wamuache aendelee na maisha yake ambayo yeye ameyachagua.
Linah alienda mbali zaidi na kuwaambia mashabiki wake kuwa wanakufuru uumbaji wa Mungu maana hata yeye akupenda awe mfupi au aonekane kama amekomaa bali ni mapenzi ya Mungu mwenyewe,hivyo amewataka mashabiki waache kuandamana juu ya maisha yake.
"Jamanii nimechoka Na kufuru zenu, hivi naomba niulize ufupi wangu, kukomaa kwangu, mkorogo wangu vinawahusu nini? Ni naomba mfatilie kazi zangu tu vingi be ni vitu vya kawaida kila binadamu kuambiwa kasoro zake! Hvi wale ambao Hawana mikono Na miguu Na wao walie vipi kwa Mungu? Namshukuru hivi nilivyo. Mbona mnapenda kutoa hukumu kama nyie ndyo Israeli?! Ifike kipindi tukumbuke kila mtu anamaisha yake! Naona mnaandamana sana Na maisha yangu."
Linah Sanga ambaye ameonyesha kuhuzunishwa sana na vitendo hivyo aliweka wazi kuwa machozi anayotoa kwa ajiri ya maneno ya watu juu ya maisha yake anamini hayatapotea bure bali Mungu atalipa kwa wale wote ambao wamekuwa sehemu ya chanzo cha machozi hayo kwake.
"Nyie ni kina baba na kina mama wa badae kumbukeni mtazaa na nyinyi halafu tuone! Chozi langu hili haliendi bure!! U will pay it back maana nimechoka na masimango yenu."
Linah Sanga amekuwa katika kundi la wasaniii ambao mashabiki wanakuwa wakiwaongelea vibaya katika mitandao ya kijamiii, kutokana na aina ya maisha ambayo wao wanakuwa wakiishi huenda ni maisha ambayo yamekuwa na makwazo kwa mashabiki hao,wakiangalia mwenendo wa msanii huyo toka alipotoka na jinsi alivyo sasa, Wema Sepetu, Shilole, Lulu Michael ni kati ya wasanii wachache ambao wamekuwa wakipokelewa tofauti katika post zao nyingi.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment