Wafanyakazi Tanesco na Wachina Wawili Wafikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Ufisadi

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Wafanyakazi wawili wa Tanesco na raia wawili wa China wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Kagera kwa tuhuma za  kutenda makosa kumi na sita na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

Watuhumiwa kutoka  Tanesco Isaack Tibita na Olver Mushumbusi kwa nyakati tofauti walikuwa mameneja Wilayani Karagwe wanadaiwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya Chico kufanya udanganyifu na kujipatia fedha hizo.

Raia wa China katika kesi hiyo ni Wang Lei na Zhang Shuaitong ambao kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa 16 wakati wa kuhamisha miundombinu ya umeme zikiwemo nguzo ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami ya Kyaka,Bugene.

Katika kesi hiyo namba 65 ya mwaka 2015 Wakili Mfawidhi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hashimu Ngole alisema watuhumiwa kati ya mwaka 2011 na 2014 kwa nyakati tofauti walitenda makosa hayo na kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Miongoni mwa makosa waliyosomewa washitakiwa ni kughushi nyaraka zikiwemo hundi za malipo zinazonyesha kuwa kampuni ya Chico imelipwa fedha kupitia mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Kyaka Bugene.

Mtuhumiwa wa tatu ambaye ni raia wa China Wang Lei  alikuwa meneja wa mradi huo na alisomewa mashitaka mawili peke yake huku mtuhumiwa wa nne Zhang Shuaitong akifanya tafsili kutokana na raia mwenzake kufahamu lugha ya Kichina pekee.

Pia wafanyakazi hao wa Tanesco miongoni mwa mashitaka mengine yanayowakabili ni kughushi nyaraka zilizoonyesha kuwa shirika hilo lilikuwa linadai kulipwa na kampuni ya Chico na kuwa kwa nyakati tofauti walipokea fedha kutokana na nyadhifa zao.

Watuhumiwa wote walikosa dhamana baada ya hakimu Charles Uiso kusema kuwa hakimu anayehusika na kesi hiyo alikuwa na majukumu mengine na itatajwa tena Desemba 7,na kupewa masharti ya dhamana.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top