Pinda Avutiwa Na Kasi ya Dr. Magufuli.....katika mazungumzo yake alijikuta akisema haya kwa watanzania..... Hii si ya kutosoma

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amesema ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim, wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi na uadilifu wao, wataivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati ambako serikali imejielekeza kufika.

Pinda amesema yeye anaona kasi hiyo ya utendaji inayochukuliwa na serikali ya awamu ya tano, ni sahihi na kinachohitajika ni kumuombea tu kwa Mungu.

Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya kufungua Kituo cha Utamaduni cha China hapa nchini katika mahojiano maalum na waandishi wa habari waliotaka kufahamu namna anavyoona kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Alisema kila rais anayeingia madarakani, lazima aingie na nguvu yake ya kufanya kazi ambayo inaweza kujenga imani kwa wananchi wake na yeye anaona sawa kasi hiyo aliyoingia nayo Dk. Magufuli.

“Unajua kila rais anayeingia madarakani, lazima aje na nguvu yake ambayo itajenga imani kwa wananchi, hivyo mimi naona ni sawa tu, kikubwa ni kumuombea tu,”alisema Pinda kwa ufupi.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top