Orodha ya majina yaliyotajwa na TRA ya kampuni na watu waliokwepa ushuru wa kontena 329

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;


Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) juzi ilitaja majina ya kampuni 43 na wamiliki wa makontena 329 ambayo yalipitishwa bandarini bila kulipiwa ushuru, na kufichuliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango alisema Mamlaka hiyo iliagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa kuchukua hatua mara moja kwa kufuatilia na kubaini wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) zilizohusika katika kashfa hiyo.

Alisema mbali na hilo walitakiwa kuwatambua wamiliki wa makontena hayo, bidhaa zilizokuwemo, kuwalipisha wahusika kodi iliyokwepwa pamoja na kuwachukulia hatua watumishi waliohusika na upotevu huo.

Dk. Mpango aliyataja majina ya makampuni na watu binafsi na idadi ya makontena waliyopitisha bila kulipia ushuru (katika mabado) kuwa ni:-

1.Lotai Steel Tanzania Ltd (100)
2.Tuff Tryes Centre Company Ltd (58)
3.Binslum Tyres Company Ltd (33)
4.Tifo Global Mart Tanzania Company Limited      (30)
5.IPS Roofing Company Limited (20)
6.Rushywheel Tyre Centre Co Ltd (12)
7.Kiungani Trading Co Ltd (10)
8.Homing International Limited (9)
9.Red East Building Materials Company Ltd (7)
10.Tybat Trading Co Limited (5)Zing Ent Ltd (4)
11.Juma Kassem Abdul (3)Salum Link Tyres (3)
12.Ally Masoud Dama (2)CLA Tokyo Limited (2)
13.Farid Abdullah Salem (2)Salum Continental Co Ltd (2)
14.Zuleha Abbas Ali (2)Issa Ali Salim (2)
15.Snow Leopard Building (2) 
16.Abdulaziz Mohamed
17.AllyAhmed Saleh
18.Tawred Ali Amer 
19.Ally Alhamdany Awadhi
20.Salim Saleh Faheed
21.Abdallah Said Hani
22.Said Hassan Hussein
23.Suleyman Hamud Suleiman Enterprise 
24.Kamil Hussein Ali Libas Fashion 
25.Nassir Salehe Mazrui Ngiloi Ulomi Enterprises Co Ltd 
26.Omar Hussein Badaway 
27.Said Ahmad Hamdan Said
28.Ahmed Said Salumu Peculiar Tyres Sapato N. Kyando Simbo Yonah Kimaro Strauss International Co. Ltd Swaleh Mohamed Swaleh

Alisema kwa ujumla, makampuni hayo yalipitisha makontena 329 ambayo yaliondolewa kinyume cha taratibu kutoka ICD ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhresa And Company Limited.

Dk. Mpango alisema bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo ni pamoja na matairi ya magari, samani mbalimbali, betri za magari, vifaa vya ujenzi, nguo na bidhaa zingine mchanganyiko.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top