Mwanasheria Mkuu Awakana Wakuu Wa Mikoa Wanaositisha Likizo Za Watumishi

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amezungumzia suala la wakuu wa mikoa kutoa matamko ya kusitisha likizo za watumishi wa umma kwa kuwataka wafanye kazi tu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha Azam, Masaju amesema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu taarifa za kuwepo matamko hayo kutoka kwa baadhi ya wakuu wa mikoa.

Amesema kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na kwamba sheria na katiba ya nchi lazima ifuatwe na watu wote nchini bila kujali cheo cha mtu aliyetoa matamko hayo.

Masaju amesema  kuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote ofisini kwake kutokana na matamko hayo ambayo amekuwa akiyasikia kwenye vyombo vya habari pekee .

Katika mahojiano hayo,Masaju alikataa kueleza moja kwa moja kama uamuzi huo unaochukuliwa na baadhi ya wakuu wa mkoa ni kosa kisheria.

“Mimi sio Jaji wa kusema kuwa waliosema hivyo wamevunja sheria, lakini nataka kusema kuwa sisi sote tunaongozwa na sheria na katiba ambavyo lazima vifuatwe.” Alisema Masaju.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla wametangaza kusitisha likizo kwa watumishi katika mikoa hiyo kwa sababu za kuwataka wafanye kazi tu

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top