Lowassa: Nilishinda Urais Lakini CCM Wakaupora Ushindi Wangu na Dunia Nzima Inajua

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Aliyekua mgombea Urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameendelea kudai ndiye mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na dunia inajua.

Katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari kupitia msemaji wake, Aboubakary Liongo, Lowassa alisema ushindi wake uliporwa na kupewa mtu mwingine lakini amewataka Watanzania wasikate tamaa.

Lowassa pia aliwashukuru Watanzania kwa kumpa kura nyingi wakati wa uchaguzi huo, kura ambazo alidai kuwa zilimfanya kuongoza dhidi ya wagombea wengine.

Hata hivyo, katika uchaguzi huo wa Oktoba 25, Rais John Magufuli ndiye aliyeshinda kwa kupata kura 8,882,935 (sawa na asilimia 58.46) na Lowassa kura 6,072,848 (sawa na asilimia 39.97) ya kura zote.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva alimtangaza Dk. Magufuli kuwa Rais mteule siku nne baadaye na aliapishwa Novemba 5, mwaka huu.

Liongo alisema Lowassa alitoa shukrani hizo juzi jioni katika mikutano ya hadhara wa kumnadi mgombea ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye kata za Mkonoo na Nodisaito.

“Nawashukuru sana Watanzania kwa kanipa kura nyingi kabisa. Tulishinda, dunia nzima inajua na wao wanajua, Watanzania mmeonyesha imani kubwa kwangu,” amekaririwa Lowassa.

“Nawashukuru sana Watanzania kwa uvumilivu wenu baada ya kushuhudia ushindi wenu ukiporwa… mlitaka wakati ule nitoe tamko muingie barabarani kudai ushindi wenu.

“Lakini nawapenda, Watanzania siko tayari kuona mnapoteza maisha,” imesema taarifa hiyo ikimkariri  Lowassa.

Aliwaomba wananchi wa Arusha kumchagua Lema katika Uchaguzi wa jimbo hilo kesho ili kuliletea maendeleo Jiji la Arusha ambalo linaongozwa na Ukawa.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top