Kafulila Aanza Vizuri Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge Baada Ya Pingamizi Kutupiliwa Mbali Na Mahakama

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;


Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo.

Katika utetezi wa mawakili wa Kafulila ambao  ni Daniel Lumenyera na Tundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi.

Jana Jaji anayesikiliza kesi hiyo Bi Leila  Mgonya alizingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.

Aidha,Jana hiyo hiyo Mahakama iliendelea na hoja ya kutathmini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.

Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipa kama dhamana utatolewa  leo na Mahakama.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top