NIACHENI N FITO ZANGU SHILOLE AWAPASHA WATU SOMA KIUNDANI

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Msanii mwanadada Shilole ambae kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa 'Nyang'anyang'a' amefunguka na kuwataka watu ambao wanamkejeli kuwa ana miguu mibaya wamuache na miguu yake hiyo.

Shilole jana alipost picha kwenye Instagram ambayo ilikuwa ikionyesha sehemu kubwa ya miguu yake na baadhi ya watu walianza kusema kuwa afunike miguu yake hiyo kwani ni mibaya wengine walionyesha kupenda picha ile huku wengine wakimpa sifa kuwa ni mrembo, lakini hizo comment chache zilionyesha kumkera Shilole kiasi cha kuamua kufunguka kwa wale ambao wana kazi ya kuwakosoa watu.

“Nyie wenye kazi ya kukosoa wenzenu, OOoh miguu mibaya mara ipo kama fito sijui nini. Niacheni na fito zangu mwenywe nimeridhika sasa kama mnataka kushindana na Mungu jiumbeni nyinyi na mapungufu yenu mliyonayo na siachi kuzianika fito zangu mbona mtakereka sanaaa,” aliandika Shilole.

Katika hatua nyingine baadhi ya mashabiki wa Shilole walionyesha kutopendezwa na baadhi ya tabia ya watanzania kuanza kukosoana na kusemana vibaya kama ambavyo wamefunguka hapo chini.

Rebecca2559: “Jaman watanzania tupunguze majungu mtu anaishi atakavyo mwacheni Shilole afanye atakacho kila mtu na maisha yake”.

Sabrasuy8: Kama wao wana miguu mizuri basi kuna walichokosa. Achana nao hawaigi kua kama wewe bali wanafikiri kuponda ndio uhodari wao, achana nao wanakukubali ila kukupongeza wanaona haya hao.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top