MSHTUKO MKUBWA! Shirika la Habari ‘lazima habari’ Z’bar

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Sehemu ya jengo la Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)
Sehemu ya jengo la Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)
SHIRIKA la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limezima kwa njia ya kupuuza “khabari muhimu” iliyohusu mkutano wa faragha wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Maalim Seif Shariff Hamad, ambao ni wa kwanza kufanyika kati yao tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Anaandika Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Viongozi hao waliogombania wadhifa wa urais kwa mara nyingine, baada ya kupambana kwa mara ya kwanza uchaguzi mkuu uliopita 2010, wamekutana wakati nchi ikigubikwa na kimya kikubwa tangu ilipoingizwa katika mgogoro wa uchaguzi.
Mgogoro huo ulitokana na tamko la kufutwa kwa uchaguzi nchi nzima lililotolewa na mtu mmoja tu – Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Shirika hilo liitwalo ZBC, ni asasi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na linaendesha stesheni ya redio ambayo ikiitwa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) na televisheni iliyokuwa ikiitwa (TvZ).

Stesheni ya redio inaitwa ZBC Radio na TvZ inatwa ZBC TV kufuatia mabadiliko ya muundo yaliyofanywa baada ya kuanzishwa shirika hilo kama asasi inayojitegemea, iliyoko chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Kiongozi wa ZBC ni Mkurugenzi Mkuu aitwaye Hassan Abdalla Mitawi, mwanahabari aliyebobea fani ya utayarishaji na usimamizi wa vipindi kwa njia ya televisheni aliyesomea elimu hiyo ya juu nchini Ujerumani.

Anasaidiwa na Naibu Mkurugenzi, Dk. Yussuf Khamis ambaye alisomea kozi ya juu ya uandishi na usimamizi wa televisheni nchini Uingereza. Yeye pia ndiye anayesimamia shughuli za siku kwa siku za ZBC Radio.

Haifahamiki ni kwanini hasa viongozi wa ZBC wamegomea taarifa ya kikao cha viongozi wakuu wa vyama vinavyoshindania mamlaka ya kuongoza Zanzibar, ambao wanaangaliwa kwa jicho kali kama ndio “watatuzi halisi” wa mgogoro huo.

Mitawi yuko karibu kiuhusiano na serikali na maofisa wa Ikulu na watendaji wa Wizara ya Habari na Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), uhusiano unaoonekana hauwezeshi ZBC kukosa habari muhimu kama hiyo ya mkutano wa viongozi hao.

Wakati Dk. Shein anataka kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano, Maalim Seif anauhakika ameshinda uchaguzi huu lakini anafanyiwa “mizengwe” na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Viongozi wa CCM wamekuwa wakitamka hadharani siku zote kwamba “Serikali iliyopatikana kwa mapinduzi, haiwezi kutolewa kwa vikaratasi.”
Maana yake ni kwamba kwa kuwa serikali ilitokana na mapinduzi ya Januari 12, viongozi wa CUF wakiitaka, “basi nao wapindue.”

Ni kauli ambayo wachambuzi wa masuala ya siasa, haki za binaadamu na wanasheria wanaichukulia kama “siasa chafu za kihafidhina” zilizolenga kuzorotesha ukuaji wa demokrasia nchini.
Kidunia, uchaguzi wa viongozi kidemokrasia, unachukuliwa kama njia muafaka ya kuipatia nchi yoyote uongozi unaotokana na ridhaa ya wananchi na kudumisha utaratibu wa kidemokrasia wa kukabidhiana madaraka kwa amani.

Kwa sababu hiyo, inaonekana kwamba kutangazwa kwa habari iliyohusu kukutana kwa Dk. Shein na Maalim Seif, ni pigo kwa jitihada za viongozi hao wahafidhina wa CCM kupigania kuhujumu ushindi wa Maalim Seif ambaye amekuwa akilalamika kuwa anaporwa ushindi ili kuzuia mabadiliko ya uongozi Zanzibar. Amelalamikia uchaguzi wote tangu ule wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi uliofanyika mwaka 1995.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top