Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu Ahoji Bunge Kuchangiwa na Makampuni ya Umma....Ampa Tahadhari Rais Magufuli Na kutaka awachukulie hatua watu hawa.....

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu amesema anatilia shaka hatua ya Taasisi muhimu kama Bunge kukusanya michango kutoka kwa Taasisi za umma ili kuendeshea shughuli zake, ikiwamo hafla ya uzinduzi wa Bunge mjini Dodoma.

Aidha, Profesa Baregu ameshangazwa na hatua ya Rais John Magufuli kupokea fedha hizo na kuzibariki kutumika katika kununulia vitanda katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuhoji malengo na msingi wa mhimili huo wa kutunga sheria kuchangiwa fedha hatua ambayo msomi huyo amedai kuwa ni kumwingiza Rais kwenye mtego wa ufisadi wa kimfumo.

“Bunge ni taasisi nyeti sana kuruhusu kuchangiwa pesa na watu au taasisi ambazo linapaswa kuzisimamia. Mara kadhaa wakuu wa mashirika haya hutakiwa kuhojiwa ikiwemo kuwasilisha matumizi yao mbele ya Kamati za Bunge; Je, kweli Bunge litakuwa na nguvu ya kuzisimamia endapo linapokea michango kutoka kwenye Taasisi hizo?” amehoji Profesa Baregu.

Profesa Baregu ameelezea kitendo cha Bunge kukusanya michango kwa ajili ya hafla kuwa ni ufisadi wa kimfumo ambao haustahili kuvumiliwa.
  
Aidha msomi huyo amesema anategemea kuwa kwa umakini alionao Rais Magufuli hatalifimbia macho hili na atawataka Bunge wajieleze ni kwa namna gani wameingia kwenye ufisadi huu wa mfumo na ikiwezekana kuwachukulia hatua wote waliohusika.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top