LIVE TOKA BUNGENI: Rais Magufuli Yuko Bungeni Kwa Ajili Ya Kulizindua na Kuhutubia haya ndo maneno yake

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Rais Magufuli mchana huu   analizindua  rasmi  Bunge  la  11  la  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  mjini Dodoma ambapo pia atatoa mwelekeo wa Serikali yake ya Awamu ya Tano katika miaka mitano ijayo.
 
Kabla  ya  kuingia  ndani  ya  ukumbi  wa  Bunge,  Rais  amekagua  gwaride  maalumu  lililoandaliwa  kwa  ajili

Awali, kabla  ya  Rais  Magufuli  kuingia  Bungeni,Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alitoa hoja ya kutengua kanuni ili kuwaruhusu viongozi wa kitaifa kuingia bungeni kushuhudia Rais Magufuli akihutubia Bunge.

Tundu Lissu: Napenda tupate muongozo kuhusu baadhi ya wageni kuwakaribisha ndani, kwa hali ilivyo leo hatuna Rais wa Zanzibar, hatuna makamu wa kwanza au wa pili halali wa Zanzibar, hatuna spika wala baraza la wawakilishi Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar muda wa serikali ya Zanzibar uliisha tangu Novemba 2.

Naibu spika amemjibu kwa kusema kifungu pia kinasema Rais wa Zanzibar anafikia ukomo mpaka Rais mpya anapoapishwa.

Update
Muda  huu  Rais  wa  Zanzibar  ndo  anaingia  Bungeni,lakini  kuna  hali  ya  vurugu. Wabunge  wa  Ukawa  wanazomea  huku  wakisema Maalim Seif...... Maalim Seif........Maalim Seif.......Maalim Seif

--> Wabunge  wa  CCM  nao  wanashangilia  huku  wakisema  CCM......CCM....CCM

Update:
Wabunge  wa  UKAWA  Watolewa  Nje  ya  ukumbi  wa  Bunge

Updates:
Rais Magufuli  ameanza  kuhutubia  bunge

-Anasisitiza  kutimiza  ahadi zake  alizoahidi
-Analipongeza jeshi  la  polisi  na  Tume  ya  Uchaguzi  kwa  kufanikisha  zoezi  zima  la  uchaguzi

-Kampongeza  sana  Zitto  Kabwe  kwa  kutozomea  na  kutoka  nje  kama  walivyofanya  wabunge  wengine  wa  upinzani

-Rais  Magufuli  anawapongeza  marais  wastaafu  waliomtangulia  kwa  nzuri  walizofanya

-Kasema  tumemaliza  uchaguzi  tukiwa  wamoja, hivyo  serikali  yake  itahakikisha  inadumisha  amani  hii  kwa  gharama  yoyote

-Rais  amesema  wakati  wa  kampeni, wananchi  walitoa  malalamiko mengi  kama Rushwa,migogoro  ya  ardhi,kuhodhi  maeneo bila kuendelezwa,uvivu, matumizi mabaya ya mali za umma, matatizo  ya  maji 

-Kasema  eneo  lingine  lililolalamikiwa  ni  Uwepo  wa  Rushwa  TRA na  ukwepaji kodi, Tanesco  kukata  umeme hovyo, watumishi wa maliasili kujihusisha  na  ujangili

-Mengine  yaliyolalamika  ni  ubovu  wa  huduma  za  afya, lugha chafu za waaguzi na tozo za ajabu

==>Mh.Spika nimeamua kuyataja haya  ili tujue pakuanzia

-Sehemu nyingine  inayolalamikwa ni uhamiaji, pia  suala  la  Elimu ambapo kuna malalamiko ya walimu na huduma mbovu kwa wanafunzi
 
-Lawama  pia  zilitolewa katika sekta ya  madini ambapo wazawa  hawanufaiki,Mizani rushwa imekithiri,Mahakamani haki zinapindishwa, uvuvib haramu, wakulima kutopewa pembejeo za kilimo

-Eneo lingine ni uchakavu wa Reli, kuzorota kwa shirika la ndege

==> Hizi  ni  baadhi  ya  kero  ambazo  nimezitaja  ili  kwa pamoja tusaidiane  kuzitafutia  ufumbuzi

Pamoja  na  kero  hizo, kuna mambo mengine ambayo tumejipanga kuyasimamia na  kuyatatua. Mambo  hayo  ni;

1. Kuulinda  muungano wetu 
2. Kumarisha mihimiri ya Serikali 
-Tumejipanga mihimiri yetu ya Bunge na Mahakama  inapata pesa za kujitosha ili iweze kufanya kazi zake kwa uhuru

3. Mchakato wa katiba mpya.
-Serikali yangu inatambua kazi kubwa iliyofanywa na watangulizi wetu pamoja na bunge la katiba lililotupatia katiba pendekezwa.Tunaahidi  kutimiza wajibu wetu kumalizia kiporo hiki tulichoachiwa

4.Uchumi na matarajio ya wananchi
  -Tutaboresha miundo mbinu  ili kuinua uchumi. Tumejipanga kuzijenga upya Reli zetu ili  kuboost vizuri uchumi wetu
-Tuna gesi na madini,tutahakikisha wananchi wote wananufaika na rasrimali hizi.

5.Ujenzi wa Viwanda
-Serikali ya awamu ya tano itaweka kipaumbele katika ujenzi wa viwanda
 -Tutaanza  na  Viwanda Vilivyopo  na  kuhakikisha vinafanya kazi
 -Waliobinafishwa viwanda hivyo  nawataka  waanze  kazi  mara moja.Wakishindwa tutawanyang'anya  mara  moja
- Tumejipanga kuhimiza  na  kushawishi  wawekezaji  kuwekeza  zaidi  nchini ili  kukuza  zaidi uchumi  wetu

Sura  Ya  Viwanda  Tunavyotaka  Kuviunda
-Sura  Ya  Kwanza: Ni vile ambavyo malighafi  yake  itatoka  ndani  ya  nchi
 
-Sura  Ya  Pili  ya  Viwanda hivi  ni  vile  vya  kuzalisha  vifaa  ambavyo  vitatumiwa  zaidi  ndani  ya  nchi

***Viwanda hivi  vitakuwa  na uhakika wa soko ndani  ya  nchi  

-Sura  Ya  Tatu  ya  Viwanda  hivi  ni  kuzalisha  ajira  nyingi  kwa  watanzania

6. Kilimo, Mifugo  na  Uvuvi
-Tutaziangalia  sekta  hizi  kwa  mtazamo  wa  kibiashara  ili  kukuza  viwanda  vyetu.
-Tutahakikisha wavuvi hawavamiwi na majambazi
-Tutafuta kodi za wakulima ambazo hazina ulazima
-Wanachi hawatanyang'anywa ardhi zao kiubabe  

7.Umasiki na Ajira
-Nakiri,pengo la wenye nacho na wasio nacho linazidi kuwa kubwa.
-Tumejipanga kupunguza umasikini  na  kukuza ajira kwa kutilia  mkazo uanzishwaji  wa  viwanda, uvuvi, mifugo  na  kilimo  kama  nilivyosema
-Tumejipanga pia  kuwawezesha  vijana  kwa  kuwaandaa  kielimu na  kiujuzi 
-Tutahakikisha vyuo vyetu vinawaandaa vijana kiufundi
-Tutawapa vijana mitaji ya kuanzisha kampuni kulingana na fani zao
-Vijana wataanzisha saccos zao na watatakiwa kujiunga na mifuko ya jamii   

==> Makundi maalumu ya Bodaboda,mamalishe na Machinga
- Ushuru  usio wa lazima kwa machinga, mama lishe tutaufuta
-Nawataka viongozi wote wa halimashauri  wasiwanyanyase  watu  hawa  kwa  namna  yoyote  ile  na  sitawavumila.

8. Afya  
-Tutaimarisha huduma za afya pale zilipo  na  kuzianzisha pale  ambapo  hazipo
-Tutawapatia mafunzo watumishi wake ndani na nchi
-Tutawapatia vifaa vya kutosha ili kuondoa ulazima wa watu kutibiwa nje
-Tutaongeza bajeti ya wiraza ya afya.

9. Elimu
-Tutaongeza mkazo katika masomo ya sayansi
-Tutahakikisha vifaa  na  maabara zinaongezwa
-Kuanzia Mwakani elimu ya shule  ya  msingi  hadi  kidato  cha  nne  ni  Bure
-Wanafunzi  wa  Vyuo  watapata mikopo kwa wakati
-Matatizo  ya  walimu yatatiliwa  mkazo

10. Maji
-Tutaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 85 vijini na 95 mijini.
 -Hatutaki akina mama kubeba ndoo kichwani.Tutaboresha miundo mbinu  ya maji

11.Umeme    
-Tutakamilisha  miradi  iliyopo na mingine mipya itajengwa ili kuhakikisha upatikaji wa umeme kwa kiwango kikubwa.
-Pale mtera kuna hujuma, watu wanafungulia maji ili yamwagike hovyo  wauze  mafuta. Naahidi kupambana Nao.

12.Madawa ya Kulevya.
-Tunaahidi  kuusaka  kwa gharama zote mtandao wa wauza madawa ya kulevyo.
-Tutashughulika na wakubwa,sio vidagaa  na  hatutawaogopa  na  mungu  anisaidie

13. Rushwa  na  Ufisadi.
-Nachukia sana Rushwa na ufisadi 
-CCM tumejengwa katika imani ya kukataa  Rushwa na Ufisadi, japo sina  imani sana kama wanachama wa  sasa hawatoi na kupokea rushwa.
-Wananchi wamechoka sana na Rushwa na hawako tayari kuvumilia UPUUZI  wa  serikali  kuwavumilia mafisadi  na  wala  Rushwa
-Dawa  ya  jipu  ni  KULITUMBUA......Nimejipa  hii kazi  ya  kuyatumbua  haya  majipu
-Nafahamu ugumu wa vita  niliyoamua  kupambana nayo  maana  Rushwa  hutendwa  na  viongozi  wakubwa  wa  nchi, lakini naamini  wananchi  wataniunga  mkono  katika  mapambano  haya  ya  Rushwa  na  Ufisadi.
-Ili  kulitatua  tatizo  hili, nimedhamiria  kuanzisha  mahakama  ya  Rushwa  na  Mafisadi
- Kiongozi  yeyote  ntakaye  mteua  na  kujihusisha  na  Rushwa  NITAMTIMUA  MARA  MOJA  na  hatua  nyingine  za  kisheria  zitachukuliwa   
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top