Bunge Laanza kwa Spidi: Nape Apigwa Dongo, Aambiwa Anasumbuliwa Na Utoto, soma hapa kujua nani kampiga dongo

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza jana mjini Dodoma na moto ambao wengi waliutabiri huku harufu ya ushabiki wa vyama ikitawala.

Katika zoezi la kumtafuta Spika wa Bunge hilo lililotanguliwa na maswali na majibu kwa wagombea nane waliojitokeza, Mgombea Uspika kupitia Chadema, Goodluck ole Medeye alikwaruzana kimtazamo na mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye.

Swali la Nape lililokuwa kati ya maswali matatu aliyoulizwa Ole Medeye lilionekana kumuudhi mgombea huyo. Nape alimtaka Ole aeleze kama ameacha tabia ya ubaguzi kwa madai kuwa Godbless Lema aliwahi kumtuhumu kuwa ni mbaguzi.

Ingawa Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Andrew Chenge alikataa swali hilo lisijibiwe akieleza kuwa halikuwa swali, Ole Medeye alihitimisha kwa kumueleza Nape alichokuwa nacho moyoni ingawa hakumtaja jina.

“Kuna mbunge hapa aliniuliza swali ambalo kwa lugha za kibunge tunaliita ni swali la kuudhi. Mbunge huyo nimemsamehe, sina chuki naye kwa sababu najua kinachomsumbua ni utoto tu, akikua ataacha,”alisema Ole Mideye.

Uchaguzi huo ulikamilika na kumuwezesha Job Ndugai kuwa spika wa Bunge hilo baada ya kupata asilimia 70 ya kura zote.
 Kwa habari za hakika na matukio ya kweli ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, kwa njanja zote SIASA, MICHEZO,BURUDANI,MAPENZI na MAKALA za science na Technology JOIN kwa Facebook group yetu iitwayo "UCHAGUZI TANZANIA" na "UTAMU WA MAISHA".
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top