TAARIFA RASMI KUHUSU MATOKEO YA UDIWANI,UBUNGE NA URAIS JIMBO LA NYAMAGANA, MWANZA

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula ametangazwa mshindi wa mbio za ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya mbunge anayemaliza muda wake, Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura 79, 280.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Nyamagana, Peter Mainya, amesema jumla ya wagombea saba walichuana kuwania nafsi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa Nyamagana.

Mainya amesema, ushindi wa Mabula umetokana na msingi uliowekwa na chama chake katika matokeo ya uchaguzi wa udiwani ambapo kati ya Kata 18 zinazounda jimbo hilo, CCM imeweza kujinyakulia Kata 14 huku Kata nne zikichukuliwa na Chadema.

“Kutokana na msingi huo, Stanslaus Mabula ameweza kupata kura 81,170. Hivyo basi, kwa mamlaka niliyopewa, namtangaza Stanslaus Mabula kuwa ndiye mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Nyamagana” alisema Peter Mainya.

Ezekiel Wenje anakuwa mbunge wa pili wa upinzani kupoteza kiti chake jijini Mwanza baada ya Highness Kiwia aliyekuwa anatetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Ilemela kuangushwa na Anjela Mabula katika matokeo yanayoashiria kurejea kwa utawala wa CCM katika siasa za Mwanza.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top