LOWASSA ATOA ONYO KALI KWA VIGOGO WA JESHI LA POLISI NA HAYA NDIO MANENO YAKE KWA JESHI LA POLISI

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;


Mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, jana alihitimisha kampeni zake mkoani hapa huku akiwatahadharisha vigogo wa Jeshi la Polisi kuwa waache ubabe kwa wananchi na kuzingatia sheria za nchi kwani wakiendeleza uonevu atawashtaki kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Mwezi uliopita, Lowassa aliahirisha kufanya kampeni kwenye viwanja vya Tangamano kutokana na watu kuwa wengi kuliko uwezo wa eneo hilo ambalo lilizidiwa na watu kadhaa waliojitokeza kuzimia kwa joto na kukosa hewa.
Akizungumza katika moja ya kampeni zake kwenye viwanja vya Indian Ocean jana, Lowassa alisema baadhi ya  polisi siyo waungwana kwani hutumia mabomu na nguvu kubwa kuwashambulia wananchi.
“Napenda kuwatahadharisha tena… nisije nikawashtaki ICC kwa kufanya vurugu na kuwapiga wananchi bila kosa. Waacheni wafanye shughuli zao,” alisema.
AHADI YA VIWANDA
Lowassa alisema endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu Jumapili ijayo, atahakikisha anafufua viwanda vyote vya Mkoa wa Tanga ili vijana wapate nafasi ya kuajiriwa. “Hili ni tatizo sugu kwa Tanga. Viwanda vingi vimekufa… hivyo naahidi nitavifufua ili vijana wapate ajira,” alisema.
Aidha, alisema akiingia madarakani ataanzisha mchakato mpya wa kuangalia ni utaratibu gani umetumika kwa ajili ya kuboresha Bandari ya Bagamoyo badala ya Bandari ya Tanga. Alisema awali, serikali ilipanga kuboresha Bandari ya Tanga, lakini fedha hizo zilipelekwa Bagamoyo.
Katika hatua nyingine, kulikuwa na taarifa kuwa Polisi walipiga mabomu kadhaa ya machozi kuwatawanya madereva wa bodaboda waliokwenda kumpokea Lowassa kwenye uwanja wa ndege.
 Mmoja wa madereva wa bodaboda, aliiambia Nipashe kuwa wakati wakielekea uwanjani, ghafla msafara wao ulizungukwa na askari na baadhi kunyang’anywa bodaboda zao kabla mabomu kupigwa.  Hata hivyo, Nipashe haikuthibitisha undani wa taarifa hizo kwani hadi tunakwenda mitamboni, hakukuwa na taarifa rasmi kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Tanga.
WAGOMBEA UBUNGE, UDIWANI
Mgombea wa ubunge wa Tanga Mjini, Musa Bakar Mbarouk, alisema Rais Jakaya Kikwete, alipoingia madarakani aliahidi kufufua viwanda vya Tanga vilivyokufa, lakini hakufanya hivyo. “Hii ni moja ya changamoto iliyopo Tanga, ndiyo maana vijana hawana ajira.
 Pia bandari yetu inafanya kazi chini ya kiwango na kusababisha wafanyabiashara kushushia mizigo yao kwenye Bandari ya Mombasa,” alisema. Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohammed, alisema zimebaki siku tatu kuingia kwenye uchaguzi mkuu, hivyo wananchi wote wa Tanga wanatakiwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa kumchagua Lowassa kwa kishindo.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinajitahidi kung’ang’ania madaraka kama kawaida yao, lakini ni lazima sasa waondoke  kupitia sanduku la kura.
“Hata waking’ang’ania madarakani, lakini lazima wataondoka tu...na dalili zote zinaonyesha kuwa wameshashindwa,” alisema.
Aliongeza: “Rushwa na ufisadi ni sehemu ya CCM.”  Mbali na kufanya kampeni zake jijini Tanga, Lowassa pia alifanya mikutano pia katika maeneo ya Ngorongoro, Loliondo, Handeni na Kilindi.
CHANZO: NIPASHE
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top