KINGUNGE APASUA JIPU NA KUVUNJA NGOME YA CCM HUKO MARA NA HII HAIJAWAHI KUTOKEA .....HII HAPA HABARI KAMILI

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare -Mwiru
MWANASIASA mkongwe Kingunge Ngombare -Mwiru, anarajiwa kufunga kampeni za Mgombea ubunge Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere (Chadema), Oktoba 24 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi mkuu. Anaandika Moses Mseti, Musoma … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa leo na Vicent Nyerere wakati na waandishi wa habari ambako amesema katika hatua hizi za mwisho wamekusudia kuvunja ngome za CCM na kujiongezea nguvu ya ushindi wa kishindo siku ya jumapili.
Nyerere ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, amesema kutokana na mwanasiasa huyo kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi ana imani ataweza kuwabadilisha baadhi ya wafuasi wa CCM na kuungana na gari la mabadiliko.
“Mzee Kingunge Oktoba 24 mwaka tutafunga nae kampeni zetu hapa Musoma, katika siku hizi za mwisho tutaweza kufanya mabadiliko makubwa sana,” amesema Nyerere.
Nyerere amesema kuwa kada huyo aliyejiengua CCM mwezi huu mwanzoni, atakisaidia Chadema kuvunja ngome zote za CCM Oktoba 24 mwaka huu siku moja kabla ya uchaguzi Mkuu.
Kingunge ambaye ni anamiliki kadi namba nane ya CCM ni miongoni mwa makada 20 wa Tanu na Afro Shirazi Part (ASP) waliounda mfumo ulioanzisha CCM.
Hata hivyo Nyerere amesema kutokana na chama chao kuwa na nguvu na mvuto kwa Wananchi wana uhakika wa kushinda majimbo yote ya mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top