HABARI KUBWA:..KAMPENI ZA CCM ZAFUNGWA HUKO MAKETE NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoa wa Njombe kimehitimisha rasmi kampeni zake hii leo kwa kuwaomba wananchi waliofika kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni hizo na ambao hawakufika kuhakikisha hawafanyi makosa kukichagua chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Akihitimisha kampeni zake mgombea udiwani kata ya Tandala (CCM) Egnatio Mtawa ameanza kwa kuwaomba radhi wananchi kutokana na kutofika kwenye mkutano huo mgombea Ubunge jimbo la Makete (CCM) Prof Norman Sigalla kutokana na kulazimika kwenda Ludewa kushiriki maziko ya aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo marehemu Deo Filikunjombe

"Kama tulivyotangaza awali kuwa Prof Norman Sigalla atakuwepo hapa kwenye kampeni lakini niwaombe radhi sana kuwa kutokana na msiba uliolipata taifa wa kuondokewa na shujaa Deo Filikunjombe kwa ajali ya helicopter amelazimika kwenda Ludewa kumzika, hivyo nawaombeni mtusamehe kwa kuwa msiba ulitokea ni wa ghafla na hakuna jinsi" amesema Mtawa

Amesema kwa kuwa anahitimisha kampeni zake hii leo amesisitiza kusimamia vipaumbele vyake ambavyo ni afya, maji, elimu na vinginevyo na kuongeza kuwa maendeleo yaliyofanyika kwa miaka mitano iliyopita na watu wakayakubali, endapo atapata ridhaa kwa miaka mitano ijayo yataongezeka mara dufu

"Ahadi zote nilizoahidi kwenye mikutano yangu ya kampeni katika vijiji vyote vinne vya kata hii ni lazima niyatekeleze, hivyo ninaomba ridhaa yenu mnichague mimi Egnatio mtawa niwe diwani wenu, Prof Norman Sigalla awe mbunge, na Dr. John Magufuli awe rais, nawaomba sana msifanye makosa" amesema Mtawa

Katika kampeni hizo katibu wa CCM kata ya Tandala Yusuph Sanga ametoa elimu kwa wananchi waliofika mkutanoni hapo jinsi ya kupiga kura ili kusaidia kura zisiharibike, kwa kuhakikisha wanawapigia kura wagombea wote wa CCM na alama ya tiki watakayoiweka wahakikishe inaenea ipasavyo katika kiboksi kilichopo kwenye karatasi
 Bibi akifuatilia maneno anayoyasema mgombea udiwani
 Sehemu ya wananchi walioshiriki mkutano huo
 Mgombea udiwani kata ya Tandala kupitia CCM Egnatio Mtawa akiwa jukwaani akinadi sera zake

 Chadema nao ndani

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top