Najua ni jinsi gani namna kulivyo na ugumu kuanzisha majadiliano haya, ukizingatia kwamba mastaa hawa wawili bado wana njaa ya mafanikio, lakini ishara zinaweza kuonekana japo kwa mbali, hivyo basi tunawaza walau kujaribu kutafsiri nini kinachomaanishwa hapa.
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamebadilisha kabisa namna ambavyo tumekuwa tukiungalia mpira. Kila wanapokuwa wanaingia uwanjani, basi wazo lao kubwa ni kuvunja rekodi za dunia hii. Na hawaonekani kanakwamba wanaweza kuacha kufanya hivyo wakati wowote hivi karibuni.
Hivi karibuni Cristiano Ronaldo alivunja rekodi na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid, huku akicheza michezo 400 pungufu ya ile aliyocheza nguli Raul ambaye alicheza michezo zaidi ya 700 kuweka rekodi hiyo. Katika ngazi ya klabu ameweza kufunga magoli 446 katika michezo 632. Ameshinda tuzo ya mchezaji bor wa dunia mara tatu (Ballon d’Or).
Lionel Messi kwa upande wake bado anaendelea kuvunja tu rekodi mbalimbali. Alivunja rekodi ya kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi katika kalenda ya mwaka, ambayo hapo awali ilikuwa ikishikiliwa na nguli wa Ujerumani Gerd Muller. Amevunja rekodi ya dunia kuwa mchezaji bora wa dunia mara nne.
Wawili hao wameshavunja rekodi nyingi sana, kiasi cha kwamba tukiziunganisha kwa pamoja zitajaza ulimwengu huu. Sasa basi, swali kubwa lililopo hapa ni kwamba, ni wachezaji gani wengine ambao wataweza kuvunja ama angalau kuzikaribia rekodi za ama kuweka changamoto kwenye mafanikio ya wawili hawa?
Hapa tuwaangazi wachezaji watatu ambao pengine wanaweza kuvunja rekodi za wawili hao (Messi na Ronaldo);
3. Anthony Martial- Manchester United
Watu wengi sana wanasema huyu jamaa anapewa sifa zisizostahili lakini kadri muda unavyokwenda watauona ukweli juu ya hili.
Katika michezo 79 aliyocheza, kinda huyo ghali kabisa kuwahi kutokea katika historia ya soka, ameshafunga magoli 19 zaidi ya Ronaldo na Messi wakati wakiwa na umri wa miaka 19.
2. Eden Hazard – Chelsea
Msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu Uingereza. Anakosa nguvu kama za Cristiano Ronaldo ama hata ufundi kama wa Lionel Messi lakini uwezo wake mkubwa wa kutembea na mpira ni wa juu mno.
Pia ana uwezo mkubwa sana wa kupiga penati (97%) zaidi ya Ronaldo na Messi. Akiwa na umri wa miaka 24, tayatri Hazard ameshafunga mabao 99 katika michezo 365 katika klabu zote alizocheza. Bado ana muda wa kufnya makubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
1. Neymar- Barcelona
Nahodha huyu wa Brazil pengine ndiye hasa mchezaji ambaye Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanapaswa kumhofia. Akiwa na umri wa miaka 23, mchezaji huyo wa zamani wa Santos ameshafunga magoli 194 katika michezo 325 katika ngazi ya klabu.
Na kama utaongeza magoli yake 46 aliyofunga katika timu yake ya taifa ndani ya michezo 67, unaweza kuona kwamba Neymar yuko mbioni kuvunj rekodi ya Pelle ambaye ndio mfungajji wa muda wote mwenye mabao 77 katika michezo 91 aliyocheza.
Kwa makadirio tu, ndani ya miaka 15 iliyobakia katika maisha yake ya soka. Messi na Ronaldo ni lazima waongeze magoli zaidi ndani ya hii miaka 5 mpaka 6 iliyobakia, lakini ikumbukwe pia na yeye atakuwa bado anafunga katika kipindi chote hicho.
Filed Under:
INTERNATIONAL NEWS,
SPORTS
on Monday, October 12, 2015
Post a Comment