CHADEMA, CCM Nusu Kwa Nusu, LOWASSA na Bandari Tanga, Baa na Uchaguzi? Hukumu Mita 200 leo! (Audio)

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;
Good Morning mtu wangu leo ni Alhamisi 22 October 2015, na kama kawaida lazima asubuhi ianze na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM. Kama zilikupita na hukuzisikia zote unaweza ukacheki na hizi nyingine hapa chini kufidia. 

CHADEMA, CCM nusu kwa nusu, Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais wa nchi… Hukumu ya kesi ya mpigakura kusimama umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura kutolewa leo na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, Edward Lowassaameahidi kusitisha mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kutumia fedha hizo kuboresha bandari ya Tanga ije kuwa na hadhi ya kushindana na bandari ya Mombasa kama tu akipewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa awamu ya tano

Mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Mama Anna Mghwira amesema akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atasimamia ukusanyaji wa kodi ili kupunguza gharama za maisha na kupambana na umasikini, kufumua mikataba ya gesi na utalii na kuiweka wazi kwa wananchi… Rais Jakaya Kikwete leo anategemea kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la wahadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam. 

Askofu wa jimbo Katoliki Morogoro, Askofu Mkude asema nchi haitokuwa na amani kamaUchaguzi Mkuu wa October 25 hautofuata taratibu za Uchaguzi kwa amani, adai wanaosema CCM haijafanya kitu chochote cha maana wanakosea kwani ukichunguza utagundua yapo mambo mengi mazuri yaliofanywa na chama hicho. 

Jaji Mkuu wa TanzaniaOthman Chande asema mwaka huu watapokea kesi nyingi za Uchaguzi kutokana na hali ya kisiasa iliyopo sasa hivi nchini na Serikali imeagiza baa zote zinazokesha kuuza bia zisitishe huduma hiyo saa sita usiku kwenye mkesha wa Uchaguzi Mkuu ili kuepusha fujo zozote zinazoweza kuibuka tarehe 25 October 2015.
 
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top