MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kogwa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, amesema iwapo atachaguliwa kuliongoza jimbo hilo kwa awamu ya nne, atahakikisha anatatua mgogoro kati ya wakulima wa Wilaya ya Kogwa na wafugaji wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
kwa mujibu gazeti la MwanaHALISI Online leo, Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika amesema: “Sababu kubwa iliyopelekea kukua kwa mgogoro huu ni mzaha, ubinafsi na uzembe uliokuwa ukifanywa na baadhi ya viongozi wa serikali wilayani Kiteto katika kusuruhisha mgogoro kati ya wafugaji na wakulma.”
“Iwapo nitapewa ridhaa ya kuiongoza Kogwa kipaumbele cha kwanza ni kurejesha amani kati ya wakulima na wafuagaji katika wilaya za Kiteto na Kogwa. Tutakaa chini na viongozi ili kutatua tatizo hili,” amesema Ndugai.
Mbali na Kauli hiyo, Ndugai pia anakubaliana na kauli ya Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa kuhusu kuunda tume ya maridhiano itakayoshughulika migogoro ya wakulima na wafugaji ili kuondokana na matatizo ambayo yamekuwa yakiwasumbua, iwapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano.
Lowassa alitoa kauli hiyo wiki iliyopita wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Soweto wilayani Kiteto.
“Wazo alilolitoa Lowassa ni zuri hasa kwa mtu yoyote anayependa amani ipatikane. Ni aibu Watanzania kuchinjana. Viongozi tutakaochaguliwa kutumikia wananchi ni lazima tukae chini ili kumaliza tataizo hili. Tunahitaji kuwa na mipango, wala hatuhitaji kuwa na fedha za kigeni kumaliza migogoro,” amesema Ndugai.
Mwaka 2014 Watanzania walishuhudia mauaji ya kutisha ya watu 10 wilayani Kiteto katika kile kinachotajwa ni mgogoro baina ya wafuagaji na wakulima ambao wanahangaika kutumia eneo la ardhi kwa ajili ya mahitaji yao
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment