BREAKING NEWZ..PIGO ZITO UKAWA...MAHAKAMA KUU IMEPIGA MARUFUKU WATU KUKAA KWENYE VITUO HATA NJE YA MITA 200.HII HAPA TAARIFA RASMI

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Mahakama kuu leo itatoa tafsiri ya kisheria kuhusu haki ya wapiga kura kukaa mita 200 baada ya kupiga kura zao.

Kesi hiyo ilifunguliwa na mgombea ubunge wa Viti Maalumu Jimbo la Kilombero kupitia Chadema, Amy Kibatala,kupitia kwa wakili Peter Kibatala wa CHADEMA kwa hati ya dharura baada ya sintofahamu kubwa kwa wananchi jjuu ya haki yao ya ulinzi wa kura.

Mbivu na mbichi tutajuwa leo.

===========================

Updates: 20 OCT 12:00HRS

Kesi hiyo sasa itasikilizwa kesho saa 3 asubuhi baada ya upande wa serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka pingamizi sababu walipokea notisi ya walalamikaji muda wa jioni hivyo hawakujiandaa.

“Mheshimiwa Jaji, tunaomba tupewe muda kwani tulipokea nyaraka hizi muda wa kazi ukiwa umekaribia kwisha hivyo hatukujiandaa, tunaomba tupewe muda kama ikiwezekana tulete majibu saa 8:30 Mchana leo kama mahakama itaona inapendeza,” alisema Wakili wa Serikali Obadia Kameya.

Kabla Majaji hawajatolea uamuzi ombi hilo walimshauri Wakili wa mlalamikaji, Peter Kibatala kubadilisha mashtaka na kumshtaki Mkurugenzi wa Uchaguzi kwani ndiye mtendaji mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala ya Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuangalia katiba Ibara ya 74, kifungu kidogo cha 7, inayosomeka “Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.”

Baada ya marekebisho hayo, kesi hiyo iliyovutia watu wengi iliahirishwa mpaka kesho saa 3

Mawakili upande wa mlalamikaji ni Peter Kibatala na Omary Msemwa, huku upande wa walalamikiwa ambayo ni Mwanasheria Mkuu na Tume ya Uchaguzi ni Obadia Kameya na Alecia Mbuya.

Katika kesi hiyo, mgombea huyo ambaye pia ni mpiga kura mwenye maslahi na uchaguzi mkuu ujao, ameomba mahakama kwa mujibu wa kifungu hicho sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 ifafanue kuhusu haki za wapiga kura.

Mlalamikaji anaitaka mahakama iseme na kutafsiri kifungu hicho kinamaanisha nini kuhusu haki hiyo kufuatia kauli iliyotolewa na NEC pamoja na Rais Jakaya Kikwete kwamba wananchi wakishapiga kura hawaruhusiwi kukaa eneo la vituo vya kupigia kura umbali wa mita 200.

Aidha, anaitaka mahakama itamke kama ni halali kwa Rais na Tume ya Uchaguzi (NEC) kuzuia wananchi kukaa kwa utulivu umbali huo ama la.

==================

Update: 23 Oct 14: 30HRSMAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA DAR ES SALAAM, IMEPIGA MARUFUKU MIKUSANYIKO KWENYE VITUO VYA KUPIGA KURA HATA NJE YA MITA 200 KWA KUWA SHERIA HAIRUHUSU KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top