Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anaamini kuwa Chelsea watapaki basi katika mchezo wao wa leo katika dimba la Etihad Stadium.
Chelsea ambao ndio wanaushikilia ubingwa wa EPL kwa sasa, wanaelekea Etihad kusaka ushindi wao wa kwanza baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 wiki iliyopita na Swansea huku City wao wakitarajia kuongeza pointi baada ya ushindi wao wa 3-0 dhdi ya West Brom Jumatatu iliyopita.
Katika mara zote mbili walizokutana msimu uliopita, Man City na Chelsea walitoka sare ya bao 1-1, hali inayopelekea mchezo wa leo kuwa mgumu, lakini Pellegrini amesisitiza kuwa wapinzani wao watapaki basi ili kutoruhusu goli siku ya leo.
“Sidhani kama utakuwa ni mchezo wa kushambulia sana”, alisema.
“Katika michezo yote ambayo tumewahi kucheza nao hawajawahi kushambulia. Wamekuwa wakilinda mno lakini ni timu hatari sana kwa mashambulizi ya kushtukiza (counter-attack).
“Sisi tutajikita katika kushambulia kama ilivyoada. Tutacheza namna ambavyo mara zote hucheza, kwa sasa nadhani ndio njia bora kwetu kupata matokeo.
“Lakini hiyo haimaanishi kuwa hatutalinda, tutajilinda ila hatuwezi kucheza mchezo wa kujihami kwa sasa , kwa sababu tutahangaika sana.
Post a Comment