Mdogo wake Lionel Messi, Matias Messi amemtetea kaka yake maarufu kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kutokana na kukosolewa kwa mshindi huyo wa tuzo nne za Ballon D’Or nchini Argentina kwa madai kwamba ameshindwa kuipa mafanikio ya timu ya Taifa.
Mara zote Messi anapoondoka Barcelona kwenda kuiwakilisha Argentina katika mashindano ya kimataifa anaibeba nchi yake mabegani mwake kama ilivyokuwa kwa Diego Maradona, lakini anakumbwa na bahati mbaya kila anapoingia kwenye mechi muhimu za mashindano.
Licha ya Lionel Messi kuonesha kiwango kizuri katika fainali za Copa America zilizomalizika siku za karibuni nchini Chile , kazi yake nzuri ilisahaulika baada ya kupoteza mechi ya fainali kwa mikwaju ya penalti na wenyeji Chile.
Nyota huyo wa Barcelona amekuwa akipondwa na mashabiki pamoja na vyombo vya habari na ikafika mahala mhariri wa gazeti za Ole alimtaka ajiuzulu unahodha.
Matias ambaye amejichora Tattoo ya kaka yake amemtetea mdogo wake akisema kwamba anakosolewa sana ikiitwa mtu wa kupoteza, lakini hastahili mzigo mkubwa kiasi hicho.
Baadhi ya Tweets za Matias Messi hizi hapa;
Post a Comment