Angel di Maria amewaambia Manchester United kwamba anataka kuhamia kunako klabu ya Paris Saint-Germain huku Laurent Blanc akisisitiza kuwa na nia ya kumnasa Muargentia huyo hata ikibidi wiki hii.
Mabingwa hao wa Ufaransa, awali walitoa ofa ya pauni milioni 46.5 na inasemekana kuwa mpaka kufikia siku ya Jumatatu dili hilo litakuwa limekamilika.
Stoo ya United ikiwa na maski za Robin van Persie, Di Maria na Radamel Falcao ambazo ndizo pekee zinazouzwa kwa bei rahisi kabisa
Kocha wa Manchester United aliwaambia wachezaji wake mapema kabisa kabla ya mchezo dhidi ya Barcelona kwamba Di Maria yuko mbioni kujiunga na PSG baada ya kukacha kujiunga na wenzake kwa ajili ya mchezo huo huko Santa Clara.
Marcos Rojo kwa upande wake hakuwepo pia lakini yeye taarifa zake ziko wazi kwamba ana matatizo katika pasi yake ya kusafiria lakini hata hivyo anaweza kukumbana na hatua za kinidhamu kutoka kwa kocha wake kutokana na uzembe huo.
Post a Comment