DALILI ZA LOWASA NA KINGUNGE KUTIMKIA UKAWA HIZI HAPA

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Image result for kingunge na lowassa

Bila shaka kwa sasa ni dhahiri shahiri kuwa mtarajiwa wa URais wa safari ya Matumaini akisaidiwa na mkongwe wa siasa nchini Kingunge Ngomare Mwiru wanaelekea kumwaga manyanga ndani ya CCM.

Kitendo cha Kamati ya Maadili ya kumchinjia baharini Rais aliyetarajiwa ndugu Edward Ngoyayi Lowasa kimeitikisa ngome ya CCM. Lowasa alikonyesha kila dalili ya kuwa Rais wa awamu ya 5 lakini wahafidhina wa CCM wamemkata maksudi ili asitimize safari ya matumaini kwa Watanzania. Kuna kila dalili zinazoashiria kuwa Lowasa akisaidiana na mkongwe Kingunge wako mbioni kuihama CCM wakti wowote kuanzia sasa.

Kauli ambazo zinaedelea kutolewa na Kingunge Ngomare Mwiru kwenye media kuwa Lowasa ndiyo alikuwa chaguo la wengi nje na ndani ya CCM zinaendelea kuivuruga CCM. Tayari baadhi ya Wanachama wa CCM wameshaanza kurudisha kadi na kujiunga na CHADEMA au ACT. Kinachosubiriwa kwa sasa ni tamko rasmi la Lowasa na Kingunge kuhitimisha kile kilichokuwa kimepangwa iwapo jina Lowasa halitopita.

Kuna uwezekano mkubwa Lowasa akajiunga na UKAWA kwenye mojawapo ya vyama viwili vinavyounda umoja huo. Aidha atatimukia ACT au CHADEMA na si CUF,NLD au NCCR. Kama itatokea hivo CCM itaendelea kuwa na hli mbaya sana na kuna hatari wakapoteza nafasi ya Urais kwa mwaka huu wa 2015.

Kama UKAWA watacheza karata zao vyema wakiwa na LOWASA na Dr. SLAA ni dhahiri John Pombe Magufuli(John Alcohol Padlocks kwa Kiingereza) hatoweza kufurukuta mbele ya miamba hawa wa UKAWA. Ikumbukwe kuwa Magufuli amezukiwa na nyota ya Jaha, kalala Waziri na kuamka akiwa Rais pasi na kufanya juhudi zozote za kuingia Ikulu. Mvutano wa Lowasa na Membe ndiyo umemnufaisha John Pombe Ma-padlocks.

Kama itatokea hivyo basi CCM itabidi wafanye kazi ya ziada ambayo si ya kawaida ili kumnusuru Magufuli asipoteze Urais. CCM itabidi safari hii wajipange sana kuwatumia TISS(UWT) na POLICCM ili kumwingiza Magufuli Ikulu ya magogoni. Nina hakika CHADEMA watakuwa tayari wana andaa NONDO wakisaidiana na baadhi ya watu wa Lowasa ambao wako ndani ya system(Serikali na CCM) ili kuhakikisha Magufuli haingii Ikulu.

Kwa CCM itakuwa kazi sana kumsafisha Magufuli kutokana na maskendo yake ya Kuuza nyumba za serikali kwa kuwagawia ndugu zake kama urithi vile, Ufisadi kwenye ujenzi wa Barabara kulingana na taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,Ununuzi wa Vivuko na Meli feki/mbovu, Ukaidi na Ujeuri wa Magufuli kuitikia wito wa Mahakama wakti wa kesi za Uchaguzi lakini pia Ukurupukaji wa Magufuli katika kutekeleza kazi zake za kila siku.

Kweli Magufuli ni mchapa kazi huku kwenye nafasi za Uwaziri kwenda chini.Kwa utendaji wa kukurupuka Magufuli atajikuta peke yake baada ya kufukuza Mawaziri, Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa Taasisi za serikali, Wakuu wa idara, Wakuu wa W/Mikoa.

Pamoja na uchapa kazi wake Dr. Magufuli lazima atatekeleza sera za CCM zilizojaa RUSHWA na UFISADI wa kila aina. Ni dhahiri hatafanya kinyume cha ilani ya chama chake lakini pia kama alivyoahidi baada ya uteuzi HATAWA ANGUSHA WALIOMWEZESHA kuukwaa Urahisi.

Lazima atalinda maslahi ya Mzee Mkapa anayenuka Rushwa lakini pia ataendeleza sera mbovu za kutetea Katiba bomu inayopendekezwa. Tumemsikia akiwa visiwani kwa ahadi kemkem za kuulinda Muungano kufa na kupona. 

Image result for kingunge na lowassa KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top